HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA UCHUKUZI ATEMBELEA TCAA



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhe. Abdallah Mitawi, ametembelea Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa lengo la kufahamu kwa kina majukumu ya Mamlaka pamoja na utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazolenga kusimamia na kuendeleza sekta ya usafiri wa anga nchini.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Dkt. Jabiri Bakari, alimueleza Naibu Katibu Mkuu kuhusu majukumu na shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Mamlaka, ikiwemo usimamizi na udhibiti wa shughuli za usafiri wa anga, usalama na ulinzi wa anga, pamoja na utoaji wa huduma kwa watumiaji wa sekta hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Mitawi ameipongeza TCAA kwa juhudi inazofanya katika kuhakikisha usalama na ufanisi wa shughuli za usafiri wa anga nchini, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha usalama wa Usafiri wa anga kwa kuwa sekta hiyo ni kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Taifa.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa Tanzania kutumia kikamilifu fursa zilizopo katika sekta ya usafiri wa anga, huku akihimiza kuendelea kuboresha huduma na miundombinu, kuimarisha ushirikiano na wadau pamoja na kutumia ubunifu na teknolojia za kisasa ili kuongeza mchango wa sekta hiyo katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Katika ziara hiyo, Mhe. Mitawi pia alitembelea maeneo mbalimbali ya TCAA na kujionea shughuli zinazotekelezwa na Mamlaka, ikiwemo Kituo cha TCAA cha Uongozaji Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Imeelezwa ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Wizara ya Uchukuzi za kufuatilia utekelezaji wa majukumu na miradi ya kimkakati katika sekta ya usafiri wa anga, kwa lengo la kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kukua, kuwa salama na kutoa huduma zenye ufanisi kwa wananchi na wadau mbalimbali.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. Abdallah Mitawi akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Dkt. Jabiri K. Bakari alipotembea katika ofisi za Mamlaka zilizopo eneo la Banana, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. Abdallah Mitawi akizungumza na baadhi ya watumishi wa TCAA wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Dkt. Jabiri K. Bakari alipotembea ofisi za Mamlaka hiyo eneo la Banana, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Dkt. Jabiri K. Bakari akitoa taarifa kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. Abdallah Mitawi alipotembea katika ofisi za Mamlaka zilizopo eneo la Banana, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. Abdallah Mitawi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Menejimenti ya TCAA ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu TCAA, Dkt. Jabiri K. Bakari pamoja na baadhi ya watumishi wa wizara ya Uchukuzi.

«
Next
This is the most recent post.
»
Previous
Older Post

No comments: