Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME - SACP
Na.
Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa
jina la Jackson s/o Venance, umri miaka 33, kabila Mhaya, mfanyakazi wa NSSF
Bukoba aliyekuwa akitembea kwa miguu pembeni mwa barabara ya Nyerere maeneo ya
TRA Dodoma katika Manispaa na Mkoa wa Dodoma amefariki dunia alipokuwa
akitibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kugongwa na gari lenye
namba za usajili T.399 CWG aina ya NISSAN iliyokuwa ikiendeshwa na Dotto d/o
Onesmo, umri miaka 25, kabila msukuma, mwanafunzi wa Chuo cha Mipango Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime – SACP amesema kabla
ya kifo chake, Marehemu alifika Dodoma kwa ajijli ya kuchukua cheti chake
katika Chuo cha Biashara Dodoma (CBE).
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kamanda Misime amesema uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajiali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari
kutokuwa mwangalifu. Uchunguzi zaidi wa ajali hiyo unaendelea na dereva
atafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia jumatatu mara baada ya taratibu
kukamilika.
Aidaha Kamanda Misime ametoa
wito kwa madereva wa Magari na Pikipiki (Bodaboda) kuwa wawe na udereva wenye
tahadhari ambao utaweza kupunguza ajali zisizo za lazima. Pia amewataka
madereva hao wakumbuke kuwa wanapoendesha maeneo ya makazi na mikusanyiko ya
watu wazingatie mwendo wao usizidi na uwe chini ya speed 50 zilizotamkwa
kisheria.
Alisisitiza kuwa atakaye
kiuka maelekezo hayo ya kisheria atachukuliwa hatua kali za kisheria.
No comments:
Post a Comment