MWANDISHI WA VITABU NA MWANAHARAKATI MASHUHURI WA MAREKANI MAYA ANGELOU, AFARIKI DUNIA

 Mshairi, mwandishi wa vitabu na mwanaharakati wa Marekani Maya Angelou amefariki akiwa na umri wa miaka 86.
Akiwa mmoja wa waandishi maarufu zaidi kwa miaka 50, Angelou anajulikana zaidi kwa kitabu chake cha mwaka 1969, I Know Why the Caged Bird Sings. Kilikuwa ni kitabu cha kwanza kati ya saba ya vitabu kuhusu maisha yake kuanzia mateso aliyopata miaka ya 1930s.
I Know Why the Caged Bird Sings, kilichoandika kuhusu ubaguzi wa rangi na mateso ya familia wakati akikua kilikaa miaka miwili kwenye orodha ya vitabu vilivyouza zaidi. Vitabu vyake vingine ni pamoja na Just Give Me a Cool Drink of Water ‘fore I Diiie (1971), And Still I Rise (1978), Now Sheba Sings the Song (1987), na I Shall Not Be Moved (1990).
Shairi lake ‘On the Pulse of the Morning’ lililoandikwa kwaajili ya sherehe ya kuapishwa kwa Rais Bill Clinton liliwagusa wengi na kuuza kopi zaidi ya milioni moja Marekani. Alipewa pia kazi ya kuandika mashairi kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Mataifa mwaka 1995 na alimkumbuka Nelson Mandela kwenye shairi kwaajili ya ikulu la Marekani mwaka jana.
Angelou pia aliongoza filamu Down in the Delta, iliyoshinda tuzo tatu za Grammy kwa album ya maneno ya kuongea.

No comments

Powered by Blogger.