Jamaa wawili wanaotuhumiwa kuwa wezi, nusura wauawe kwa kuchomwa moto na raia wenye hasira kali baada ya kula kichapo ‘hevi’ kwa msala wa kukwapua mkoba wa mrembo aliyekuwa ndani ya Bajaj.
Alisema baada ya kupora mkoba huo walianza kutoka nduki lakini kabla hawajafika mbali, mtu mmoja aliyekuwa na gari, ambaye pia aliona tukio hilo, aliziba njia na kuwafanya vijana hao kutumbukia mtaroni.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Katika tukio hilo lililojiri maeneo ya Kijitonyama, Dar, mwanzoni mwa wiki hii, shuhuda aliyeona alisema aliwaona vijana hao wakiwa wamepanda pikipiki wakipora mkoba wa mrembi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Magdalena John (21).
Msichana huyo alishuka ndani ya Bajaj na kuanza kuwapigia kelele za
wizi hivyo kuwafanya wapita njia kuanza kuwapiga kwa kutumia silaha
mbalimbali zikiwemo mawe, fimbo na matofali. Waandishi wa habari hii waliowahi kufika eneo la tukio, waliwashuhudia watu hao wakipokea kipigo kikali kilichowafanya wawe hoi.





No comments:
Post a Comment