Taaluma na mfumo wetu unaweza kuwa tofauti kidogo
ila mambo huwa yanakwenda kwa mlinganyo fulani ambao unatakiwa kuufahamu, hasa
kwenye taasisi binafsi ambazo kinachoangaliwa ni utendaji na uwajibikaji
madhubuti. Kwenye kila taaluma unaweza ukaamua kuwa abiria wa kawaida ambaye
unatizama dereva anafanya nini na unakuwa unafurahia kwa sababu wewe huhusiki
katika nyadhifa za juu. Ila kwa dereva (mmiliki, wakurungenzi) yeye huhakikisha
anaongoza kila kitu kinakwenda kama kinavyotakiwa. Kama unataka kuwa dereva au
abiria jukumu ni la kwako, unachukua maamuzi gani? Unapotaka kufanikiwa
kitaaluma hebu fuatilia watu waliofanikiwa kitaaluma wanafanya nini;
1. Unatakiwa ujue kwamba wewe ni
bidhaa au biashara ya mtu
Taaluma yako
ina mtaji ndani yake, hivyo unatakiwa kujua una amini kama mtaji katika taaluma
yako, nani anaweza kukulipa zaidi ya mwingine? kama hauna taaluma inayohitajika
ni bora uanze kutafuta ya kwako ambayo ambayo watu watakulipa kwa ajili ya hiyo
taaluma.
2. Unatakiwa kujua namna ya kutumia
fursa vizuri
Unatakiwa ujue namna ya kukubaliana
has a kwenye mshahara wake. Mwajiri anatafuta mtu atakaye mtumia kwa bei nzuri,
na wewe uwe makini sio kubebwa tu kwa hela yoyote. Kumbuka hufanyi kazi
kwaajili ya mwajiri ila unafanya kazi pamoja na mwajiri.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
3. Fanya kazi zako vizuri
Kumbuka kufanya kazi vizuri ni bora
kuliko kufanya kitu kipya. Zingatia kujenga na kuboresha ujuzi na ufanisi wake.
Unatakiwa uwe unajua baadhi ya vitu vizuri sana.
4. Fanya kazi na watu ambao wamekuzidi
uwezo
Tafuta watu waliokuzidi uwezo na
ufanye kazi nao. Tafuta makampuni ambayo yanafanya kazi kwa viwango via juu,
ujue namna ambavyo hutoa huduma zao, au bidhaa za na ukiweza tanya nao
uhusianao kibiashara ili uweze kukua namna ya utendaji katika kazi au huduma.
5. Fuatilia malengo na dira ya
Kampuni
Kama unataka uwe mtu uliyefanikiwa
kitaaluma hutakiwi kwenda kichwa kichwa au bila kujua dira na malengo ya
kampuni hiyo. Unatakiwa ujue kampuni hiyo inatekeleza malengo yapi na ni nini
dira yao ili uweze kufanya kazi na kutoa huduma kulingana na mule wanakokwenda.
Ukiweza kufanya vizuri zaidi ya pale wanapofikia uwezekano wa kukuweka katika
viwango vizuri zaidi ni rahisi. Wanahitaji mtu ambaye anajua wapi wanakwenda na
mtu ambaye anaweza kutoa huduma kulingana na vigezo vyao.
6. Uwe kwenye nafasi ambapo mambo
yasipokwenda vizuri uondoke
Jitahidi upate mshahara au fedha ya
kukutosha kukaa mwaka mzima bila kazi, kwa kuwa kila kazi ni ya muda tu unaweza
ukaipoteza wakati wowote. Hivyo ukitaka kuacha kazi hakikisha kifedha unaweza
kukuaa muds mrefu bila kuingiza kipato na mambo yakaenda.
7. Unahitaji uzoefu wa kukuwezesha
kwenda mbele zaidi
Hakuna
kushindwa ambako mtu hushindwa kabisa, tunapata uzoefu, tunajifunza na kukua
kitaaluma. Achana na kufanya kazi sehemu ambazo unajua hautafukuzwa au
hautaacha kazi hive karibuni hizo ni dalili za kwamba utapata wakati mgumu wa
kusonga mbele kitaaluma kama unataka kufanya maamuzi magumu. Unahitaji
kujifunza vitu vipya, kukosea ndio kunakufanya uweze kujifunza na kuendelea
mbele.
Je unamiliki taaluma yako? au watu
wengine ndio wanamiliki taaluma yako? Amua leo kumiliki taaluma yako mwenyewe
kwa kufanya maamuzi sahihi na kusonga mbele. Uwe tayari kuacha kazi na hiyo
ofisi uende ukafanye kitu bora zaidi kuliko hicho.




No comments:
Post a Comment