Mama yake na Ronaldo akifuta machozi
Kama Mungu angekuwa na mpango tofauti, leo hii kusingekuwa na mchezaji nyota wa soka aitwaye Cristiano Ronaldo.
Mama mzazi wa mchezaji huyo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno amekiri kuwa alijaribu kufanya abortion wakati alipokuwa na ujauzito wake. Kwenye kitabu cha maisha yake kilichozinduliwa Ijumaa hii nchini Ureno, Dolores Aveiro amedai kuwa madaktari walikataa kuitoa mimba yake.
Katika hamu kubwa ya kutaka kuitoa, alianza kunywa pombe kali na kufanya mazoezi magumu ili itoke lakini hakufanikiwa.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mama yake na Cristiano Ronaldo, Dolores Aveiro akiwa kwenye uzinduzi wa kitabu chake kipya jijini Lisbon, Ureno
Kwa mujibu wa Daily Star, mama yake Ronaldo alidai kuwa mwanae pia alikuja kufahamu kuhusiana na tukio hilo.
Akiongea kuhusu alichokisema Ronaldo baada ya kugundua hilo, mama huyo alisema: “Angalia mama, ulitaka kunitoa na sasa mimi ndiye ninayeisadia familia.”
No comments:
Post a Comment