HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » VIONGOZI WA CHADEMA MKOANI KIGOMA WAJIUNGA NA ACT

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA), Jafari Kasisiko (katikati) Katibu wa Mkoa  CHADEMA, Msafiri Wamalwa (kushoto),  Katibu wa BAWATA Bi. Malunga Simba wakiwa wanatangaza uamuzi wao wa kujitoa CHADEMA mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).

Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema) Jafari Kasisiko , Katibu wa mkoa Msafiri Wamalwa na Katibu wa Baraza la wanawake, Bi. Malunga Simba wa chama hicho Mkoa wa Kigoma wametangaza kujizulu nafasi zao na uanachama wa chama hicho na kuachia nyadhifa zao kuanzia 2014 Julai 18
Akitangaza uamuzi huo kwa niaba ya wenzake mbele ya waandishi wa habari mkoani Kigoma, Mwenyekiti Jafari Kasisiko, amesema yeye na wenzake wamefikia uamuzi huo baada ya kuona kuwa CHADEMA kimepoteza sifa ya kuwa chama cha kidemokrasia na kuwa chama cha kibabe.
“Sifa kubwa ambayo ilikuwa imetufanya tuendelee kubakia Chadema ni kwamba kilikuwa bado kinaendelea na sifa ya kuwa ni chama cha kidemokrasia, lakini baada ya kufikia hatua sasa kwamba kimeanza kuwa chama cha kibabe zaidi na kuanza kukiuka misingi ya demokrasia, kwa kweli sina sababu na wenzangu ya kuendelea kubaki katika chama hichi,”alisema.


ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Mzee Kasisiko ambaye aliondoka CCM mnamo mwaka 1985 na kukaa nje ya siasa kwa muda kabla ya kujiunga Chadema mwaka 1994, alitoa mfano unaoonesha CHADEMA, kukiuka misingi ya demokrasia kuwa ni suala la aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, ambaye alivuliwa wadhifa wake kufuatia kutangaza nia ya kutaka kugombea moja ya nafasi za juu ndani ya chama hicho.
“Mheshimiwa Zitto, kosa lake pekee ni kwa sababu alionesha nia ya kutaka kugombea uenyekiti wa Chadema. Lakini ukipitia katiba ya Chadema tangu ukurasa wa kwanza mpaka wa mwisho, hupati mahala panaposema ni kosa mtu kutamani kugombea nafasi yoyote katika chama.”
“Yeye kuonekana kuwa alikuwa na nia ya kutaka kugombea, na kikubwa zaidi tayari alikuwa na watu wanaoumuunga mkono, na mimi nikiwa mmoja wao, basi hili lionekana ni dhambi kubwa sana.”
“Kwa hiyo katika Chadema tulikuja kugundua kwamba kumbe uenyekiti sasa hivi, ukiacha uenyekiti wa zama za Mtei, uenyekiti zama za Makani lakini uenyekiti chini ya mheshimiwa Mbowe ni kitu nyeti ambacho hatakiwi mtu mwingine kugusa.”
“Kwa hiyo kitendo hichi kwetu sisi kilionesha wazi kuwa Chadema wamefikia mahala sasa hawako tayari kufuata taratibu za kidemokrasia.”
Alisema pamoja na kwamba na wamechukua muda mrefu kabla ya kutangaza uamuzi huo walikuwa na sababu za msingi ambazo ziliwafanya wasitangaze, lakini tangu siku Zitto Kabwe alipovuliwa nyadhifa zake walikuwa hawana imani tena na chama kwa sababu hawawezi kuwa ndani ya chama ambacho ni mamlaka ya watu Fulani.
Kwa upande wake Msafiri Wamalwa alisema kwa ridhaa yake bila kushawishiwa na mtu ameamua kuondoka Chadema na kwamba kabla ya uamuzi huo alikaa chini na kutafakari, wakati Malunga Simba alisema ameamua kutoka Chadema kwa sababu ni chama ambacho hakina faida na wananchi.
Baada ya kujiuzulu uongozi na uanachama wa Chadema, Mzee Ramadhani Kasisiko alisema anajiunga na chama kipya cha siasa cha Allience for Change and Transparency, ACT, lakini wenzake hawakuzungumzia kama kuna chama wanachohamia ingawa Msafiri Wamalwa alisema atatafuta chama makini.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: