Paulina Nyoni (Mama wa mtoto Fatuma Msuya) akiwa amembeba mwanaye ambaye anahitaji msaada wa matimabu .
Paulina nyoni mkazi wa kijiji cha Hanga wilaya
ya Namtumbo mkoani Ruvuma anaomba msaada kwa yeyote atakaye guswa na tatizo la
mwanaye aitwaye Fatuma Msuya ili aweze
kupata matibabu katika hospitali ya KCMC moshi.
Paulina ni mama mwenye watoto wa tano anayejishugulisha
na kilimo , Mume wake aitwaye Jafari Msuya
amemtelekeza baada ya kujifungua mtoto mwenye tatizo hili na kukimbia
kusikojulikana hivyo kumfanya mama wa mtoto huyu kutokuwa na msaada wowote ule,
Fatuma Msuya (1) amezaliwa tarehe
24/2/2013 katika Hosptali ya mkoa wa Ruvuma akiwa na tatizo la kutokuwa na sehemu ya kutolea haja kubwa na hivyo
kulazimika kufanyiwa upasuaji tumboni ambapo kwa sasa anatolea haja kubwa,awali
kabla ya kupasuliwa alikuwa akitolea haja kubwa sehemu ya aja ndogo.
Upasuaji wa awali alifanyiwa katika Hospitali
ya Mission Peramiho iliyopo wilaya ya songea tarehe 19 04/ 2013
Na kwa sasa mtoto huyu anakabiliwa na
tatizo jingine la kutokwa na vidonda sehemu anayojisaidia hali inayomsababishia maumivu
wakati wote na anapojisaidia haja kubwa hutokwa na damu.
Gharama za matibabu zinazohitajika ni shilingi milioni tatu, Yeyote atakayeguswa
anaweza kutoa msaada kwa Mpesa no 0767 710 113 .
“Kutoa ni moyo”
No comments:
Post a Comment