Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza
mwanafunzi wa kidato cha nne Neema Steven Mtwanga (16) anayesoma katika shule ya
sekondari Naboti Makambako,Njombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika
utunzi wa insha katika shindano lililoandaliwa na Jumuiya ya uchumi ya
maendeleo kusini mwa Afrika (SADC).
Rais Kikwete alimpongeza mwanafunzi huyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika mji wa kitalii wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe ambapo mwanafunzi huyo aliandika insha inayohusu mabadiliko ya tabia nchi. (Picha na Freddy Maro)
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu na wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa jumuiya hiyo uliofanyika katika hoteli ya Elephant Hills mjini Victoria Falls Zimbabwe leo.Katikati ji mwenyeji wa Mkutano huo Rais Robert Mugabe na mkewe Grace Mugabe.
No comments:
Post a Comment