BREAKING NEWS: MSAFARA WA MAALIM SEIF WAPATA AJALI

 Makamu wa kawanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamadi.
Habari zinasema msafara wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamadi umepata ajali ukihusisha magari mawili ya msafara wa kiongozi huyo ambayo jumla yake yalikuwa saba yalipogongana na lori lenye tela.

Katibu wa CUF Wilaya ya Nyamagana, Rehema Mwenda amejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando (kulia) na muonekano wa gari (kushoto) baada ya ajali katika wilaya ya Misungwi, jijini Mwanza.

Akizungumza na mtandao huu, Mkurughenzi wa Habari wa CUf, Adam Kambaya alisema  Viongozi wawili wa CUF, katibu wa wilaya ya Nyamagana na mwenyekiti wa mtaa wa Nyamagana  ambao hakuwataja majina wamelazwa katika Hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi.
 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 Mkuu wa kitengo cha habari Wilaya, Mh Shido ambae pia ni Mwenyekiti wa Mtaa Utemini Kata ya Mirongo amejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando.
 Moja ya gari ambalo lilikuwa kwenye msafara wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu Mkuu wa Cuf, Maalim Seif Sharif Hamadi baada ya kupata ajali, Misungiwi, Mwanza leo.
 Hili ni gari lingine ambalo lenye usajili namba T397ANU nalo lilihusika katika ajali hiyo leo.
Msafara wa Maalim Seif ukijiandaa kuondoka mara baada ya magari mawili kati ya saba yaliyokuwa kwenye msafara kupata ajali.  CHANZO: GPL

No comments

Powered by Blogger.