Askari Polisi wakiwa eneo la tukio ikiwa ni kuimarisha ulinzi
(Picha Zote na demasho.com)
(Picha Zote na demasho.com)
Eneo la tukio likiwa limezungushiwa alama na Jeshi la Polisi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwangu akizungumza jambo na waandishi wa habari katika hoptal ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuwatembelea majeruhi hao
Kamati ya ulinzi na Usalama wakiwa Hospital ya mkoa wa Ruvuma.
Aliye lala kitandani ni WP ambaye amejeruhiwa akiwa amelazwa katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma
Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr Daniel Malekela akizungumza na wandishi wa habari hopitalini hapo.
Askari Ramadhani Ally akiwa anaelezea jinsi mkasa huo ulivowakuta wakiwa kazini
-------------
ASKARI watatu wa jeshi la Polisi wamelazwa
katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma (Homso) iliyopo mjini
songea Mkoani humo wakiwa wanapatiwa matibabu ya majeraha ambayo
waliyapata baada ya kushambuliwa kwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni Bomu la
kurushwa kwa mkono.
Tukio hilo limetokea September 16, 2014
majira ya saa moja na nusu jioni katika kata ya Msufini karibu na daraja la
Matarawe, wilayani Songea Mkoani Ruvuma ambapo watu watatu wasiofahamika walitupa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono
ambalo limetengenezwa kienyeji na kuwajeruhi askari hao watatu
waliokuwa doria.
Askari hao waliojeruhiwa ni WP. 10399 PC
Felista aliyejeruhiwa mguu wa kulia kwenye unyayo na pajani ,G.
7351 PC Ramadhani aliye jeruhiwa mguu wa kulia karibu na goti na tumboni upande
wa kulia na G. 5515 pc John aliyepata majeraha katika mguu wa kulia
chini ya goti na jeraha dogo tumboni.
Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr. Daniel
Malekela ameeleza kutoa vipande vya bati na misumari katika majeraha ya askari
hao na mpaka sasa wanaendelea na matibabu.
Alisema kufutia hali hiyo Jeshi la Polisi mkoani
Ruvuma linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwakamata wahusika wa
tukio hilo kwa hatua zaidi za kisheria.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe. Saidi Mwambungu kasema amesikitishwa sana na kitendo
hicho cha wahalifu kujeruhi askari tena kwa makusudi na amesema serikali kupitia
vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata.
No comments:
Post a Comment