Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME - SACP akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME - SACP amesema tarehe
25/09/2014 alfajiri vimeokotwa vipeperushi maeneo mbalimbali mjini Dodoma
vyenye ujumbe ufuatao ONYO – DODOMA SI
MAHALI PA KUFUGA WEZI WA FEDHA ZA UMMA. UTAKAYEINGIA BUNGENI KUANZIA KESHO,
YATAKAYOKUPATA UTAJUTA.
Kamanda MISIME amesema tumeendelea
kupokea taarifa za watu wanaodaiwa kuandaa vipeperushi hivyo na tunafanyia kazi
ili tuweze kuwakamata ili washtakiwe kulingana na kosa walilolitenda hasa la
kutoa vitisho na kuhamasisha uvunjifu wa amani.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Aidha Kamanda MISIME ameongeza ametoa wito
kwa wananchi na wageni wanaofika Dodoma watii sheria bila shuruti. Kila mmoja ajiepushe kujiingiza kwenye
kuhamasisha uvunjifu wa amani, kujiingiza katika mikusanyiko isiyo halali na
maandamano ambayo yameshapigwa marufuku na Jeshi la Polisi. Atakayekiuka na kujiingiza katika vitendo
hivyo vya kiuhalifu atashurutishwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria za Nchi
na kwa mamlaka iliyopewa Jeshi la Polisi.
Kamanda MISIME ameongeza kuwa wananchi na
wageni wapenda amani waendelee na shughuli zao kama kawaida kwani Jeshi La
Polisi limejiimarisha ipasavyo kukabiliana na yeyote yule atakayekiuka sheria
na maelekezo yaliyotolewa.
No comments:
Post a Comment