HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » KAMPUNI YA CANADIAN SOLUTIONS TRADING&CLEANING Est WATAMBULISHA TILES AINA MPYA ZISIZOKUWA NA UTELEZI KWENYE SOKO LA TANZANIA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

 Wakurugenzi wa Kampuni ya  Canadian Solution Trading&Cleaning Est  Kutoka kulia ni Nale Nat Alyalei(Director) akifuatiwa na Mustafa Said,Khadija Naif Alyafa(Chairwoman) na Wa mwisho kushoto Naji Ahmed akifuatilia utambulisho wa bidhaaa inayouzwa na kampuni yao.
 Mr Thoamas Toka Canadian Solution Trading&Cleaning Est  Akielezea namna jinsi moja ya Bidhaa yao ambavyo haisiki maji kwa namna yoyote ile pindi tu inapokuwa imelowa au kupata unyevu.

 Wageni waalikwa na Wadau wakifuatilia kwa makini Maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mr Thomas
 Kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est Juzi imetambulisha Aina Mpya Ya Tiles kwenye soko la Tanzania ikiwa na kauli ya  "SURE STEP" ndani ya Hotel ya Double Tree Jijini Dar es Salaam..Aina mpya hiyo ya Tiles ni mpya Tanzania kwani ni aina ambayo haina utelezi wakati wote hata pindi ikiwa na maji au Imelowa kwa Mvua au Unyevunyevu.Sure Step inafanya Kazi Vipi?akiongea na wageni walioalikwa na wadau mbalimbali Bwana Thomas amesema kuwa Tiles Hizo zina ubora wa hali ya juuu ikiwemo Garantii ya Mwaka Mmoja mpaka Mitatu.Pia akaongeza Tiles hizo pindi zitumikapo haziwezi kuharibu sakafu  wala kuweka nyufa,pia ni rahisi kusafisha pindi tu zinapochafuka kwani zimetengenezwa kwa mfumo ambao haziwezi kunyonya uchafu wa aina yoyote ile.Bwana Thomas akaongeza kuwa pia Bidhaaa hiyo ni rafiki wa mazingira kwani haina aina yoyote ya kemikali na pina zinaweza kutumika kwa matumizi ya ndani na nje.Aina za Tiles zilizotambulishwa jan ni pamoja na Stay Clean NS30,Stay Clean NS60 na Stay Clean NS90.
Bwana Thoma alisisitiza kuwa nia ya kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est  kutambulisha Tiles hizo Nchini ni kuongeza Usalama wa watumiaji wa maeneo mbali mbali ikiwemo Hoteli,Migahawa,Mjumbani,sehemu za Burudani na Maofisini Bwana akatoa mfano kuwa Nchini Canada kumekuwa na kesi nyingi za watu kuvunjika miguu kupata maumivu kutokana na matumizi ya Tile ambazo zina utlezi Pindi tu zipatapo maji Au unyevu,Hivyo akatoa uwito kwa makampuni mbalimbali ya Ujenzi Tanzania na Nje ya Tanzania kutumia Bidhaa zao ambazo ni salama na rafiki kwa matumizi ya Binadamu.
  Wageni waalikwa na Wadau wakifuatilia kwa makini Maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mr Thomas
 Wadau mbalimbali wakiwa makini kusikiliza na Kusoma kila kilichokuwa kinaelezwa na Mr Thoma toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est Jana Kwenye Hoteli ya Double Tree Jijini Dar
 Mr Thomas toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est akionyesha mfano wa kitambaa ambacho ukimagia maji hakilowi wala kushika maji ikiwa ni kuelezea namna bidhaa zao zilivyo
 Wageni waalikwa na Wadau wakiendelea kufuatilia
 Mustapha Said Toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est akiwakaribisha wageni waalikwa  kwenda kwenye meza kuu kujione kwa macho ni namna gani bidhaa zao zinavyofanya kazi.
 Mr Thoma toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est Akiwanyesha kwa vitendo wageni waalikwa na wadau mbalimbali namna bidhaa zao zinavyofanya kazi kwenye mazingira tofauti.
 Wageni waalikwa Wakiendelea kupata maelezo na kuuliza maswali kwa Bwana Thomas  toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est jinsi bidhaa zao zilivyo na zina ubora gani
 Maelekezo yakiendela toka kwa Bwana Thomas kwa wageni mablimbali
 Wageni mbalimbali na wadau wakijaribu wenyewe ili kuweza kudhibitisha kile alichokuwa anaongea Bwana Thomas kuhusu Tiles zao.mpya ambazo hazina utelezi
 Wakurugenzi wa kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est Toka Kushoto ni Chair Woman Khadija Naif Alyafa akifuatiwa na Mustapha Said,Nala Nait Alyafa(Director) na Wa Mwisho Kulia ni Naji Ahmed
 Bwana Thomas Ikabidi atoke nje na wageni waalikwa  na wadau ili kuweza kuwanyosha kwa uhalisia kabisa namna bidhaa zao zilvyo
 Wadau wakijalibu kukanyaga Tiles na Kuona kama Zinateleza ama Vipi ndani ya Hoteli ya Double Tree Jijini Dar wakati wa utambulisho wa Tiles Mpya Toka Kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est
 Hii ni Bidhaa iitwayo STay Clean Ceramic
  Hii ni Bidhaa iitwayo STay Clean NS90
   Hii ni Bidhaa iitwayo STay Clean NS60
  Hii ni Bidhaa iitwayo STay Clean NS30

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: