Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya
Kwaluguru wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vitatu vya
maabara katika shule ya sekondari Kwaluguru wilayani Handeni.
Wananchi
wa kata ya Kwaluguru wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma
Kinana wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa maabara tatu za
masomo ya sayansi katika shule ya sekondari Kwaluguru ambapo vyumba 83
vya maabara vinajengwa wilayani Handeni.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka zege kwenye moja
ya vumba vya maabara za shule ya sekondari Kwaluguru.
Mbunge
wa Jimbo la Handeni Dk. Abdallah Kigoda ambaye pia ni Waziri wa Viwanda
na Biashara akishiriki kuweka zege kwenye moja ya vyumba vya maabara
vya sekondari ya Kwaluguru.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiujenzi wa ofisi ya CCM
Tawi la Kweinjugo kata ya Kwaluguru wilaya ya Handeni
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa Handeni kwenye uwanja wa mkutano Soko la Zamani Chanika.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akicheza ngoma ya asili ya wazigua .
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Handeni
kwenye uwanja wa mkutano Soko la Zamani Chanika ambapo aliwaambia
wajifunze kupima mambo ya viongozi wa siasa wasije wakaingizwa kwenye
matatizo bila kutarajia kwani wapo zaidi kwa ajili ya maslahi yao
binafsi na si ya wananchi ndio maana wanadiriki kutangaza maandamano
wakati wao wenyewe hawapo wameenda nje ya nchi kupumzika.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Tanga Henry Shekifu akisalimia wakazi wa Handeni kabla
ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Handeni
ambapo aliwaambia watu wanatakiwa kupewa fursa na kurahisishiwa maisha
yao hivyo kodi ndogo zinatakiwa ziangaliwe upya kwani zimekuwa kero kwa
wafanyabiashara ndogo ndogo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na madereva wa boda boda wa Chanika Handeni.
Watu wakiwa wamemzunguka Katibu Mkuu wa CCM mara baada ya kumaliza mkutano wake Soko la zamani Chanika wilayani Handeni.
No comments:
Post a Comment