Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilal akihutubia wakati akifungua mkutano huo.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Shaban Lila (kulia) na Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jaji mstaafu Thomas Mihayo wakifuatilia mkutano huo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Alex Mfungo akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukanjangwa, akizungumza na wanahabari.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal (kulia), akipitia hutuba hiyo. Kulia ni Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jaji mstaafu Thomas Mihayo. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akiwa meza kuu na viongozi wengine. Kutoka kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Shaban Lila, Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jaji mstaafu Thomas Mihayo, Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Asah Mwambene na Kamishna wa Jeshi la Magereza anayeshughulikia Sheria, Dk.Juma Malewa.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo.
Washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo ulioandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT)
Dotto Mwaibale
MAKAMU wa Rais Dk Mohammed Garib Bilali ameviambia vyombo vya ulinzi na usalama kuwa waandishi wa habari si maadui wao.
Hivyo amevitaka vyombo hivyo kushirikiana kwa karibu na kuelimishana kipi kinapaswa kuandikwa na kipi hakipaswi kuandika.
Dk.Bilali alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana katika Mkutano wa mashahuriano kati ya vyombo vya Habari Tanzania na vya vyombo vya ulinzi, usalama na sheria.
Alisema kuwa vyombo vya habari vinajukumu la kulinda amani na utulivu wa nchi na kutangaza umadhubuti wa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi ndani na nje ya mipaka.
Pia alisema sekta ya habari inatanuka na kwa Tanzania wanatakiwa kuanza kufikiria namna ya kupata waanishi watakaobobea katika aina fulani ya habari kama sekta ya kilimo,afya,elimu pamoja na sekta ya gesi na mafuta.
''Tupo katika maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani na vyombo vya ulinzi vio katika mikakati ya kuhakikisha tunavuka salama katika matukio hayo lakini pamoja na hayo naomba vyombo vya ulinzi na usalama vitambue kuwa waandishi si maadui wao hivyo shirikianeni kwa maendeleo ya nchi yetu'' alisema Dk Bilali
Alingeza watumie mkutano mkutano huo kufungua ukurasa wa mahusiano na pia kutumia mkutano huo kuelimishana kuhusu majukumu yao juku wakitambua kuwa wao ni wananchi wa Tanzania na waambiane kuhusu mipaka yao na maeneo wanayoweza kushirikiana ili wafanye kazi bila kukwaruzana.
Hata hivyo alisema anaamini masuala ya ulinzi na usalama yana unyeti wake hivyo wanatakiwa kuelezana kuhusu yapi yanatakiwa kuandikwa kwa lengo la la kutoa taarifa kwa wananchi na yapi yanatakiwa kuhifadhiwa ili kutotoa taarifa kwa watu wasiolitakia taifa mema.
No comments:
Post a Comment