Mratibu wa Mpango Maalumu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Renatus Kihongo (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu mwitikio dhidi ya ukimwi kwenye barabara za kimataifa nchini kupitia vituo vya maarifa. Kulia ni Ofisa Habari wa TACAIDS, Godlease Malisa na Ofisa Habari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TACAIDS, Nadhifa Omar.
Ofisa Habari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TACAIDS, Nadhifa Omar akiongea jambo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Ofisa Habari wa TACAIDS, Godlease Malisa.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
TUME ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imeandaa mpango wa kujenga vituo vya maarifa kwa ajili ya huduma ya utoaji elimu ya kuhusu ukimwi kwa madereva wa masafa marefu.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Mratibu wa Mpango Maalum, Renatus Kihongo, alisema madereva na wasafirishaji wa mzigo inayopelekwa masafa marefu hutumia muda mrefu kukaa mbali na familia zao hivyo kuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo.
Hali ya maambukizi katika nchi kwa tafiti zilizofanyika mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Manyara imekua ikiongoza kwa maambukizi.
"Hali hii inasababisha maingiliano ya kingono baina ya wasafirishaji na wenyeji wa eneo husika na pia makundi ya wauza ngono ili kujipatia kipato,"alisema.
Alisema hadi sasa vituo ambvyo vimekamilika ni 14 katika maeneo ya barabara kuu ambapo malori hayo yanalala
Vituo hivyo ni Kagongwa Kahama,Kibaingwa Kongwa,Mdaula Bagamoyo Uvinza na Kazuramimba ,Kasula na Benacco.
Aidha vituo vingine ni bandari ya Temeke Dar es Salaam,Chalinze Makambako Tunduma,Mbozi -Mbeya Ilemela-Mwanza.
Aliongeza kuwa ujenzi wa vituo hivyo utaendelea kuongezeka hadi kufikia 21 lengo likiwa kutokomeza ukimwi katika nchi zote zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara na nchini.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment