Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge(katikati) akiwa na Viongozi wa Forum CC, kutoka kulia ni Oscar Munga, Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya ForumCC, Vera Mugita, Afisa Miradi, Fazal Issa na Adam Anthony.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith Mahenge wa kwanza kushoto akizungumza na Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya ForumCC, Vera Mugita na Afisa Miradi wa ForumCC Fazal Issa.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Meneja Ushawishi wa Oxfam, Eluka Kibona wa kwanza kushoto akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani Septemba 23, 2014Mahenge.
Afisa Miradi wa ForumCC, Fazal Issa akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari
Waandishi wa habari wakifuatilia ufafanuzi kutoka kwa viongozi wa asasi za kiraia kuhusu Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko New York-Marekani Septemba 23, 2014
Asasi Nne zisizo
za kiserikali zinazojishughulisha na kupambana na mabadiliko ya tabianchi
nchini ForumCC, CAN, YouthCAN na Oxfam Tanzania zimetoa tamko la pamoja kuhusiana
na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika huko
New York-Marekani tarehe 23/09/2014.
Katika tamko
hilo ambalo pia limewasilishwa kwa Waziri
wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Dr. Eng. Binilith
Mahenge, mambo matano yamependekezwa kuzingatiwa
wakati wa mkutano huo ambao Rais wa Tanzania DK. Jakaya Kikwete pia atatoa
hotuba yake.
Mambo hayo ni
pamoja na kupunguza utoaji wa hewa ukaa (Emission Reduction), Misaada ya Fedha
za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (Climate Finance), Kuongeza mapambano
ya mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo, Matumizi ya teknolojia na Nishati
Mbadala na Kilimo.
Picha zote na tabianchi blog
No comments:
Post a Comment