UNATAKA KUFANIKIWA? HAKUNA NJIA YA MKATO KATIKA MAFANIKIO
Je huu ni ukweli kwamba hakuna njia ya mkato kuelekea mafanikio? Inawezekana unasema ‘Awali hujui mambo yanayoendelea na utabakia hivyo hivyo’. Kuna kitu nimeendelea kujifunza kwa watu matajiri wanaochipukia kwenye Forbes magazine na kwingineko.
Siku chache zilizopita katika Kongamano fulani ambako Mjasiriamali wa Kenya Julian Kyula na Heshan De Silva waliongea kutokana na uzoefu na historia ya Maisha yao. Kitu kimoja cha kufanana ni kutumia kile ulichonacho na uweze kukiendeleza kufikia kule unakotaka.
Hakuna Njia ya Mkato kwenye Mafanikio; Kama kuna kitu ambacho hatutaweza kuendelea ni kupitia njia za mkato. Njia za mkato haziwezi kujenga maendeleo yako wala hutoweza kuacha kitu kiuchumi. Kwanini? Kuwa na fedha ambayo huna maelezo nayo au haujaiwekeza kwenye njia sahihi ni kupoteza hiyo mali.
Mimi huangalia zaidi upande chanya zaidi kuliko upande hasi, kwa kila mtu ambaye namtolea mfano naangalia upande chanya, kama una kitu hasi juu ya yeyote huo sio upande wangu wa makala hii.
Kuna njia nyingi za utafutaji wa mafanikio “kama kupanda na kuvuna” kitu ambacho watu wengi wanapenda, vilevile biashara za njia ya mitandao ili upate kamisheni kwaajili ya watu wanaojiunga chini yako. Hizo hazijawahi kuwa njia sahihi za kufanikiwa mara nyingi zinaishia kutapeliwa.
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kufanya kazi kwa umakini na sio kwa nguvu. Umakini unaozungumziwa hapa ni kuwa na watu sahihi au mtandao sahihi wa watu kuhusu biashara au bidhaa unayoifanya. Umakini huo utakusaidia kufikia malengo yako, haimaanishi kwamba hautakutana na vikwazo mbalimbali ila je una umakini gani kupambana na vikwazo hivyo?
Inabidi Ukuze kitu ulichonacho. Watu wengi tunaogopa kuchukua hatua ya kuamini kwamba kitu ulichonacho kinaweza kuwa kitu kikubwa cha kuweza kukutengenezea ajira yako na watu wengine. Tunakuwa na sababu nyingi na za kutosha kuonyesha kwamba haiwezekani. Ila ukweli uko hivi kwako haiwezekani ila kuna mtu sehemu fulani usiyoijua wewe kimewezekana. Hivyo inategemea mtazamo wako ukoje. Vitu vingi tunavyovifanya sasa hivi wazee wetu hawajawahi kufikiri kwamba vitawezekana lakini vinafanyika na wanaona vinawezekana, hivyo badilisha unavyofikiri unaweza ukabadiisha matokeo ya vitu unavyofanya kila siku. Nuia Kukua kimtizamo na kiutendaji.
Sisi sote ni matokeo ya maamuzi tunayofanya kila siku kuhusu maisha yetu, hivyo mwenye maamuzi ni wewe mwenyewe kufanya kilicho sahihi au kuamini na kufanya kulingana na habari za mtaani.
Tag:
No comments:
Post a Comment