Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Chama cha wananchi CUF leo kimetangaza kuunga mkono
harakati zinazofanywa na chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA za kuandaa
maandamano nchi nzima kupinga kuendelea kwa bunge maalum la katiba na kusema
kuwa chadema kipo sawa na maandamano hayo ni halali na watatoa ushirikiano wote
katika maandamano hayo.
Akizungumzaa jumapili hii na wanahabari jijini Dar es
salaam mwenyekiti wa chama hicho Profesa IBRAHIMU LIPUMBA amesema kuwa CHADEMA
kama chama cha siasa ni jukumu na ni haki yao kufanya maandamano pale ambapo
wataona kuna ubadhilifu wa fedha za wananchi unatokea katika nchi.
Aidha LIPUMBA akizungumzia sakata la kuitwa na
kuhojiwa kwa mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Mh
FREMAN MBOWE amesema kuwa hakuna sababu yoyote ya msingi ya kumhoji kiongozi
huyo kwani maandamano yote yanayoitishwa na CHADEMA yanafwata taratibu
zote ila kinachotokea ni polisi
kutokujua sheria za maandamano. Na kusema kumwita Mh. Mbowe ni kumdhalilisha kiongozi huyo mkubwa wa
upinzania wakati anatekeleza haki yake ya kikatiba.
“kazi ya polisi sio kuruhusu maandamano ya chama
chochote, sisi tunatoa taarifa tu kwa polisi ili watulinde,na hatuombi kibali
cha polisi kiufanya kibali, polisi wanadhani kuwa sisi tunaomba kibali cha
maandamano wakati ni haki ya kikatiba kabisa ya kuandamana na kufanya mikutano
ya adhara.
Mh LIPUMBA amesema kuwa CHADEMA sio chama cha kwanza
kutangaza maandamano ya nchi nzima kuhusu jambo la katiba kwani mapema baada ya
hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa wakati anafungua bunge la katiba chama cha
mapinduzi nao walitangaza mikutano na maandamano nchi nzima ambayo hayakupingwa
na polisi ila anashangaa upinzani kunyimwa haki hiyo ya msingi.
No comments:
Post a Comment