Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Watanzania
waendelea kufaidika kutoka kwa hospitali ya Apollo iliyoko nchini India.
Hii ni kufuatia hosiptali hiyo kufanikiwa kuwatenganisha mapacha wa
kike Abriana na Adriana waliokuwa wameunganika chini ya
kifua na tumboni kutoka nchini Tanzania katika upasuaji uliofanyika
tarehe 17 Novemba 2014 nchini India. Mapacha waliounganika kwa mtindo
huu hujulikana kwa watalaam kama Thoraco Omphalopahus na upasuaji uliofanyika na hospitali Apollo ulikuwa wenye mafanikio na wa aina yake.
Mapacha Abriana na Adriana awali
ya upasuaji huo walikuwa wameunganika kuanzia chini ya kifua na tumbo,
hali kadhalika walikuwa wakitumia mvungu mmoja wa moyo na maini
yaliyounganika. Changamoto ya upasuaji wa mapacha hawa kwa madaktari
ulikuwa kufanya utenganishaji bila kuwavujisha damu nyingi ambayo
waliweza kukabiliana nayo ipasavyo kutokana na madaktari waliokuwepo
wenye wataalum wa kiufundi na matibabu.
Upasuaji
huo ulifanywa na jopo la watalaamu 50 waliobobea katika taaluma mbali
mbali za tiba ya afya ya kabla na baada ya upasuaji ambao uliendelea kwa
masaa 11. Watalaamu walifanikiwa kutenganisha viungo vilivyo kuwa
vimeungana lakini mapacha hawa walipona na kupata ahueni kwa haraka hivo
kusaidia zoezi zima la uponyaji baada ya upasuaji.
Hali
kadhalika, hatua nyingine ya muhimu katika upasuaji huo ilikuwa
kurudisha viungi husika katika mahala pake baada ya kuvitenganisha.
Akizungumzia kuhusu hili Dkt. K S Sivakumar Plastic & Reconstructive Surgeon anasema,
“Baada ya upasuaji, moyo wa moja ya mapacha ulitakiwa kurudishiwa
mahali pake ili kuzuia mbenuko na uharibifu pamoja na maini yaliyokuwa
yameungana. Ilichukua majopo mawili ya wataalum kwa masaa nne
kukamilisha ufungaji wa maini, moyo, na utumbo katika mahala pake.”
Upasuaji
huu wa mafanikio wa mapacha waliounganika kutoka ncini Tanzania sio wa
kwanza kufanywa na hospitali ya Apollo. Mwishoni mwa mwaka 2013 mapacha
wengine wakiume waliokuwa wameungana na kujulikana na wataalamu kama Pygopagus, Ericana & Eluidi
kutoka Tanzania walifanikiwa kutenganishwa na wataalamu wa hospitali
hiyo. Matukio amabayo yamepandisha chati na kuipa hadhi ya juu hospitali
ya Apollo iliyoko nchini India na nchi ya India kwa ujumla kama
kiongozi katika sekta ya afya na mfano wa kuigwa na nchi nyingine
ikiwemo Tanzania. Hospitali hiyo ina mahusiano mazuri na nchi ya
Tanzania ikitembelewa idadi kubwa ya wagonjwa kutoka Tanzania kutokana
na ukosefu wa huduma muhimu na za kisasa nchini.
Wapacha
walioungana hutambuliwa na kupewa majina kutokana na jinsi muungano huo
unapokuwa katika viungo mbali mbali vya mwili. Ikiwa aina ya mapacha
waliounganika wa Thoraco Omphalopagus ndio inayoongoza kuripotiwa kwa
asilimia 28% zaidi ya aina nyingine zote zinazotambulika matukio mengi
yakitokea zaidi Kusini-Magharibi mwa bara la Asia, Africa and Brazili.
Katika aina hii mapacha wanakuwa wameunganika kuaznia kifuani mpaka
chini ya kifua kwenda kwenye tumbo na hutumia baadhi ya sehemu ya moyo,
ini na baadhi ya sehemu viungo vya mmeng’enyo wa chakula(i).
Kulingana
na hospitali ya Apollo kesi zinazohusu mapacha waliounganika huwa ni
nadra mathalan moja kati ya uzao 200,000 huonekana. Lakini, asilimia 60
ya hao hufariki wakati asilimia 35 hufariki katika kipindi kifupi baada
ya kuzaliwa kutokana na sababu mbali mbali (ii).
Akizungumzia upasuaji huo uliokuwa na mafanikio, Dkt. Prathap C Reddy, Mwenyekiti na Muanzilishi wa Hospitali za Apollo
anasema, “Nikitazama katika mwaka huu wa 2014 naona maisha ya watu
tuliweza kuyagusa kwa namna njema. Mbali na maumivu wanayopata watoto
yatokanayo na ugonjwa, wazazi pia hupitia mshituko na mahangaiko
makubwa. Nchi nyingi za bara la Afrika zinakosa tiba muhimu na mbadala
na hivyo kujikuta wanakuja nchini India kupata huduma hizo muhimu na
kisasa. Inafurahisha na kuleta faraja kuwa katika sikukuu hii ya
Krismasi Jimmy na Carolyn watarudi nyumbani na watoto wao wakiwa ni
binadamu wawili tofauti.”
Tangu mwaka
2007, jozi nane za mapacha waliounganika katika ini na utumbo kutoka
sehemu mbali mbali nchini India zimeripotiwa kutenganishwa. Aradhana na
Stuthi ni jozi pekee ya mapacha waliwahi kutenganishwa kwa upasuaji
wakiwa na mioyo iliyo katika mvungu (cavity) mmoja hali sawa na mapacha
Adrianan na Abriana. Japo moja ya mapacha wa thoraco opmhalopagus
Aradhana kufariki wiki tatu baadae, Adriana and Abriana na ndio aina hiyo ya mapacha walioweza kuishi baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutenganishwa.
Baada ya
miezi ya matibabu, mapacha Adriana na Abriana kutoka Dar-es-Salaam
watarejea nyumbani Tanzania tarehe 18 Disemba na kufika mjini Dar es
Saaam asubuhi ya tarehe 19 Disemba. Katika kipindi hiki cha sikukuu
itakuwa shangwe kwa wazazi Jimmy na Carolyn wanaporudi nyumbani kutoka
nchini India wakiwa na watoto wao wawili waliotenganishwa.
No comments:
Post a Comment