Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia, amesema leo Jumatano Desemba 17, 2014, kuwa hatajiuzulu ng’o kutoka wadhifa wake, kufuatia kashfa ya kuvurugika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini Jumapili iliyopita.
Waziri Ghasia, akitoka kwenye chumba cha mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza nao.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Waziri Ghasia na katibu mkuu wa TAMISEMI, Jumanne Sagini
Serikali imetengua uteuzi wa Wakurugenzi sita wa Halmashauri, na kuwasimamisha kazi wengine watano kupisha uchunguzi, kutokana na kubainika kuchangia kuvurugika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika tarehe 14, mwezi huu.
Akitangaza hatua hiyo kufuatia ripoti iliyoibua madudu yaliyofanyika katika uchaguzi huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Hawa Ghasia amesema uamuzi huo pia umeridhiwa na Rais Jakaya Kikwete.
Mhe. Ghasia amewataja
wakurugenzi hao waliotenguliwa uteuzi wao kuwa ni
1.
Bwaba Benjamin A. Majoyo ambaye ni mkurugenzi Mtendaji
wa halmashauri ya Mkuranga,
2.
Bwana Abdalla Ngodu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliuwa,
3.
Bwana Masalu Mayaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kasulu,
4.
Bibi Goody Pamba, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Serengeti,
5.
Bwana Juliusi A.
Madiga, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema na
6.
Bwana Simon C. R. Mayeye , Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bunda
i)
Bw.Felix T.Mabula, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Hanang’
ii)
Bw.Fortunatus Fwema, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbulu
iii)
Bi.Isabela D.Chilumba, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ulanga
iv)
Bi.Pendo Malabeja, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kwimba
v)
Bw.William Z. Shimweta, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Sumbawanga
i)
Bw.Mohamed
A.Maje, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rombo
ii)
Bw.Hamis Yuna, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Busege
iii)
Bw.Jovin A.Jungu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Muheza
i)
Bw.Isaya Mngulumi , Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilala
ii)
Bw.Melchizedeck Humbe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Hai
iii)
Bw. Wallace J. Karia, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Muheza
Na Pamoja Blog
No comments:
Post a Comment