Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mtu mmoja Timotheo kweka  (30) mkazi wa  kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro amekutwa chumbani kwake amefariki dunia siku nne ziizopita na jeshi la polisi limelazimika kuvunja mlango na kutoa mwili huo .
Akizungumza na ITV mmiliki wa nyumba alikokuwa amepanga Leonard Benedicti  amesema kwa mara ya mwisho marehemu alionekana nje  siku ya jumamosi hadi leo  walipohisi harufu nzito chumbani kwake  ndipo walitoa tarifa kwa jeshi la polisi na kumkuta ndani amefariki na kichwa kikiwa kimebanwa  kwenye stuli.
Wakizungumzia tukio hilo ndugu wa marehemu wamesema  hawanawasiwasi na kifo cha ndugu yao kwani  alikuwa mlevi wa pombe  kwa muda mrefu ambapo wamesema siku ya jumamosi walikuwa na sherehe ya ukoo lakini marehemu hakuweza kufika ingawa hawakujua kama amefariki.
Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limedhibitisha  kutokea  kwa tukio hilo ambapo mwili wa  marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya mkoa wa morogoro.
CHANZO: ITV TANZANIA




No comments:
Post a Comment