Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka sita amefanyiwa visa vya kinyama na
mama yake mzazi, ambaye anadaiwa kumjeruhi vibaya kwa kumchoma moto
mikono yake na kisha kumfungia ndani kwa siku nne akiugulia majeraha
bila kutibiwa wala kula chakula.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, mama
aliyefanya ukatili huo (jina linahifadhiwa) ni mkazi wa mtaa wa Eden,
Manispaa ya Sumbawanga, mkoani hapa.
Inadaiwa mama huyo alifanya kitendo hicho baada ya kukasirishwa na
kitendo cha mwanae huyo kupakua maharage kutoka kwenye chungu na
kuyala.
Ilielezwa kuwa mama huyo alikuwa ameyapika maharage hayo kwa ajili ya mlo wa mchana.
Kamanda Mwaruanda alisema mama huyo alikamatwa na polisi Desemba 13,
mwaka huu, saa tisa mchana kufuatia taarifa za siri kutoka kwa raia
wema kwamba alikuwa akimnyanyasa mwanae huyo ambaye anasoma chekechea
mjini hapa .
“Kufuatia taarifa hizo za siri askari polisi walifika nyumba kwa
mtuhumiwa huyo saa tisa mchana na kumkuta mtoto huyo akiwa amefungiwa
ndani akiugulia maumivu makali mikononi mwake baada ya kujeruhiwa
vibaya na kuchomwa moto na mama yake mzazi” alisema.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Kwa mujibu wa mtoto huyo, alifanyiwa kitendo hicho baada ya kurejea
nyumbani akitokea shule akiwa na njaa kali kwa kuwa tangu asubuhi
alikuwa hajala chochote siku hiyo.
“Mie nasoma chekechea njaa ilikuwa imenibana, nilikuwa sijala chochote
tangu asubuhi, hivyo niliamua kupakua maharagwe yaliyokuwa ndani ya
chungu ambayo yalikuwa yamepikwa na mama yangu, mama alirejea nyumbani
na kunikuta nikila maharage hayo alikasirika na akachukua fimbo na
kuanza kunicharaza.”
“Nililia sana kwa maumivu lakini mama hakunihurumia, alichukua kamba
akanifunga mikono yangu kisha akachukua kijinga cha moto akaanza
kuniuunguza viganja, nilihisi maumivu makali sana,” alisema mtoto huyo
huku akitokwa machozi.
Alisema baada ya kufanyiwa ukatili huo, bila matibabu yoyote wala
chakula, akimkataza kutoka nje kwa siku nne hadi alipookolewa na
askari polisi na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Kamanda Mwaruanda alisema mama huyo atafikishwa mahakamani mara tu baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment