Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mratibu wa tuzo za uongozi bora wa bodi katika sekta za benki na bima,
Bi Neema Gerald (wa pili kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani) katika mkutano na vyombo vya habari uliofanyika jijini Dar es
Salaam jana, kutangaza uzinduzi wa tuzo za uongozi bora wa bodi katika
sekta za benki na bima, ambazo zitamulika na kutambua mchango wa uongozi
uliotukuka wa bodi za wakurugenzi kwenye sekta za benki na bima nchini.
Tuzo hizo zimepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam January 30, 2015.
Ameambatana na Bw. Laurence Mwangoka (wa kwanza kulia), Meneja Mauzo wa
Serena Hotel ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo pamoja na
wawakilishi kutoka Capital Plus International (CPI), Bw. Matthew Kasonta
(wa pili kushoto), na Bw. Kassim Malela (kushoto).
Bw. Matthew Kasonta (katikati), mwakilishi kutoka Capital Plus
International (CPI) ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo za uongozi bora
wa bodi katika sekta za benki na bima akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) katika mkutano na vyombo vya habari uliofanyika jijini
Dar es Salaam jana, kutangaza uzinduzi wa tuzo za uongozi bora wa bodi
katika sekta za benki na bima, ambazo zitamulika na kutambua mchango wa
uongozi uliotukuka wa bodi za wakurugenzi kwenye sekta za benki na
bima nchini. Tuzo hizo zimepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam January
30, 2015. Ameambatana na Bw. Laurence Mwangoka (wa kwanza kulia),
Meneja Mauzo wa Serena Hotel ambao ni moja kati ya wadhamini wa tuzo,
Mratibu wa tuzo hizo, Bi. Neema Gerald (wa pili kulia) na mwakilishi
kutoka Capital Plus International (CPI) Bw. Kassim Malela (kushoto).
TUZO za Bodi yenye Uongozi Bora ijulikanayo kama Best Board Leadership Award (BBLA), ambazo zimelenga kutambua uongozi bora wa Bodi za Wagurugenzi katika sekta ya kibenki na bima, zimepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi ujao. BBLA iliyopangwa kufanyika mwezi Januari tarehe 30 na kufanyika kwa mara ya kwanza nchini, inaandaliwa chini ya mwamvuli wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) na Chama cha Makampuni ya Bima Tanzania (ATI).
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam jana, Mratibu wa BBLA Bi. Neema Gerald alisema tuzo hizo
zinatoa fursa ya ufahamu wa jinsi gani bodi bora inaweza kusaidia
taasisi kupata mafanikio na kufikia utendaji bora hususani katika eneo
walilobobea kiutalaam.
Wadhamini wa tukio hilo la kipekee ni pamoja na Capital
Plus Internaional Limited, Real PR Solutions Limited, Afrimax Strategic
Partnerships Limited, Serena Hotel na IPP Media, wakati wadhamini
wengine wakiaswa kujitokeza zaidi kuunga mkono tuzo hizo.
"Tumeona umuhimu wa kutambua na kuthamini mchango unaotolewa na wakurugenzi wa bodi katika taasisi zao.Tunaamini kuwa katika kila mafanikio ya taasisi ya kifedha, nyuma yake kuna bodi ya wakurugenzi imara na makini. Sasa, sifa hizo ambazo wajumbe wa bodi wengi wanakuwazo zinapaswa kutambuliwa na kuthaminiwa, "alisema.
Bi. Neema alisema kuwa utamaduni unaojulikana ni kuwa ni Maafisa Watendaji Wakuu na Wakurugenzi Wakuu pekee ndiyo wanaothaminiwa na kutambuliwa na waajiriwa au jamii nzima kwa ujumla. "Ni wakati muafaka sasa kwa bodi zenye utendaji bora kutambuliwa na kuzawadiwa kikamilifu kwa jitihada zao," alisema. Alibainisha kuwa zoezi hilo, tathmini na upangaji wa mwisho wa matokeo utafanywa na jopo la majaji waliobobea na wenye rekodi bora za kiutendaji.

Tathmini
hiyo italenga zaidi katika ufanisi wa Bodi ya
Wakurugenzi katika suala la utawala wa taasisi, usimamizi wa fedha na
uwezo wa kuiongoza dira ya taasisi kwa ujumla wake. Maeneo mengine ni
umakini wa bodi katika uwazi, uwajibikaji, utendaji, na ufuataji wa
hatua madhubuti na utendaji wake.
Alitaja maeneo mengine ambayo bodi itafanyiwa tathmini kuwa ni utoaji wa mitazamo yakinifu ya bodi katika kusisitiza umuhimu wa utendaji wa mtaji watu katika ngazi ya bodi na kuweka mbele vigezo vitakavyowezesha utendaji bora zaidi wa bodi, "alisema.

Aliongeza kuwa tuzo hizo zimeanzishwa kwa wakati muafaka
nchini wakati ambapo sekta za Bima na kibenki zinapitia mabadiliko
makubwa na kujitokeza kwa makampuni mengi ya bima na masoko zaidi
kuongezeka ili kufikia wateja wengi katika nyanja zote za maisha.
"Kwa mabadiliko haya wakati huu, hasa katika sekta ya fedha
ambapo idadi kubwa ya makampuni ya bima na mabenki zimekuwa zikifungua
biashara Tanzania, wateja wanahitaji kuwa na uhakika kuwa malipo yao ya
bima yako salama na wanaweza kupatiwa kwa wakati wowote", alisema, na
kuongeza:
"Hili litafanikiwa tu endapo kampuni hiyo ya bima au benki
itaendelea kufanya kazi kwa mafanikio. Kwa maana hiyo, bodi ya
wakurugenzi itakuwa na jukumu muhimu katika kuhakikisha kampuni hiyo
haifi, "alisema.
No comments:
Post a Comment