Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Meli ya MV Victoria inayofanya safari zake kutoka mkoani Kagera
kuelekea jijini mwanza imezuiliwa kuondoka mjini bukoba kutokana ubovu
ilionao hali ambayo imewalazimu wananchi waliokuwa wanataka kusafiri na
meli hiyo kuandamana hadi kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera
kwa ajili ya kutoa malalamiko yao.
Wakiongea nnje ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongela
wananchi hao wamelalamikia kuto kuwepo kwa usafiri wa meli kwa zaidi ya
mwezi moja sasa na kwamba jana meli hiyo imewasili mjini Bukoba na
kuambiwa wapakie mizigo yao ndani ya meli hiyo kwaajili ya kuisafirisha
kutoka mkoani kagera kueelekea jijini Mwanza ambapo wamesema wamepakia
mizigo yao ndani ya meli hiyo na leo wameambiwa meli hiyo haitosafiri
kutokana na meli hiyo kuwa na hitilafu tangu muda mrefu na kwamba mazao
yao biashara sasa yamekuwa yakiharibika ndani ya meli hiyo hali
Ambayo imewalazimu wananchi hao kuandamana mpaka kwenye ofisi za mkuu wa
mkoa wa kagera kwaajili ya kutoa malalamiko yao juu ya meli hiyo.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Akizungumza na wananchi hao mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi.Sipora
Pangani amewataka wananchi hao kuwa na subira na kuwataka waondoke
katika ofisi hizo huku akisema kuwa serikali italishughulikia suala
hilo huku mbunge wa viti maalum Conchesta Rwamulaza akiitaka serikali
kuiondoa meli hiyo kwakuwa imekuwa ikileta hofu kubwa kwa wananchi wa
mkoa huo na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake meneja wa SUMATRA mkoa wa Kagera Alex Katama
amesema meli hiyo ilisimamishwa kufanya kazi tangu ilipo pata
hitilafu kwa ajili ya matengenezo lakini juzi meli hiyo iliondoka jijini Mwanza hadi mjini Bukoba bila Ruhusa kutoka kwenye mamlaka husika na
akaongeza kuwa meli hiyo sasa ni mbovu na haifai kutoa huduma yoyote
mpaka itakapo fanyiwa marekebisho.
No comments:
Post a Comment