Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
<![endif]-->Askari
Polisi wakiondoka na sanduku la kupigia kura baada ya Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa katika Mtaa wa King’azi Kata ya Kwembe jijini Dar es Salaam kuvunjika leo kutokana na vurugu zilizowahusisha
mawakala wa CCM na Chadema na kusababisha masanduku manne ya kupigia kura
kuvunjwa. (Picha na Francis Dande)
Askari
Polisi wakiondoka na sanduku la kupigia kura baada ya Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa katika Mtaa wa King’azi Kata ya Kwemba jijini Dar es Salaam kuvunjika leo kutokana na vurugu zilizowahusisha
mawakala wa CCM na Chadema na kusababisha masanduku manne ya kupigia kura
kuvunjwa.
Msimamizi wa Uchaguzi katika Kata ya Kwembe aliyetambulika kwa jina moja la Magwiza (kulia) akitoa maelezo kwa maofisa wa Polisi waliofika katika kituo hicho baada ya kutokea vurugu.
Hali ilikuwa hivi nje ya chumba cha kupigia kura baada ya maofika wa polisi kufika.
Kamanda E.M. Tille akizungumza na simu ili kupata muhafaka wa kituo hicho.
Maofisa wa Polisi wakijadiliana jambo.
Baada ya msimamizi wa uchaguzi kuahirisha uchaguzi huo maofisa wa polisi na wadau wengine wakitoka nje.
Msimamizi wa uchaguzi, Magwiza (katikati) akitondoka baada ya kuahirisha uchaguzi huo mpaka baada ya miezi mitatu.
Wafuasi wa Chadema wakipaza sauti baada ya uchaguzi kuahirishwa.
Wafuasi wa Chadema wakiwa katika mkusanyiko baada ya uchaguzi kuahirshwa tena kwa muda wa miezi mitatu.
Wafuasi wa Chadema wakiwa katika mkusanyiko baada ya uchaguzi kuahirshwa tena kwa muda wa miezi mitatu.
Askari wakiondoka katika eneo la tukio.
Na Mwandishi Wetu
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Na Mwandishi Wetu
*Polisi Dar waondoka na
maboksi ya kura baada ya kuvurugika
*Mabomu ya machozi
yarindima
Na Mwandishi Wetu
UCHAGUZI wa marudio wa
Serikali za Mitaa, uliofanyika sehemu mbalimbali nchini leo, umeibua vurugu kubwa
pengine kuliko hata zile zilizotokea kwenye uchaguzi wa Desemba 14 mwaka huu.
Katika maeneo mengi nchini,
uchaguzi huo wa marudio umevunjika na vurugu kubwa zimetokea kiasi cha
kusababisha Polisi kuingilia kati na kurusha mabomu ya machozi.
Sababu za kuvunjika kwa
uchaguzi wa jana zinafanana na zile za Desemba 14 za uzembe wa wasimamizi wa
uchaguzi ambao ni wakurugenzi wa halmashauri ambapo wakurugenzi sita wa
halmashauri walitimuliwa kazi, watano kusimamishwa, watatu kupata onyo kali na
watatu onyo la kawaida kwa madai ya kusababisha kuvurugika kwa uchaguzi huo.
Katika uchaguzi uliofanyika
katika Mtaa wa King’azi Kata ya Kwembe wilayani Kinondoni, jijini Dar es
Salaaam, umeahirishwa tena kwa mara ya pili baada ya kutokea vurugu.
Vurugu hizo zimesababisha
wanachama watatu wa Chama Cha Maendeleo (Chadema), kukamatwa na polisi kwa
madai kuwa ndio chanzo cha kuvurugika kwa uchaguzi huo.
Kauli ya kuahirisha
uchaguzi huo, ilitolewa jijini jana na Msimamizi
Msaidizi wa Uchaguzi huo, aliyetambulika kwa jina moja la Magwiza.
Magwiza, alisema ameamua
kuahirisha uchaguzi huo baada ya kubaini kutoweka kwa amani katika eneo hilo
kutokana na mvutano uliotokea kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chadema.
Chadema walisema hakuna
sababu ya kurudia uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa kwani alikwishapatikana Desemba
14 mwaka huu ambapo Donath Mtemekele (Chadema), aliibuka mshindi.
Viongozi wa Chadema, walisema
kwa kuwa katika uchaguzi wa kumpata mwenyekiti wa Mtaa wiki iliyopita ulikwenda
vizuri na mshindi kupatikana kihalali, lakini uchaguzi wa wajumbe ndio
uliovunjika, hivyo hakuna sababu ya kurudia uchaguzi wa nafasi Mwenyekiti.
Katika uchaguzi wa wiki iliyopita,
Mtemekele wa Chadema alipata kura 312 na
mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Eric Mandani aliambulia kura 207 na mawakala wote
waliridhika na matokeo hayo ya nafasi ya Mwenyekiti.
Wakati Chadema wakipinga
uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti
kurudiwa, CCM nao walipinga wakitaka uchaguzi wa nafasi hiyo pia urudiwe kama
ule wa nafasi za wajumbe ambao wiki iliyopita haukufanyika kabisa.
Vurugu zilizuka baada ya
kuanza kuhesabiwa kura za wagombea nafasi za ujumbe.
Aliyeanzisha vurugu hizo
alikuwa Mandari wa CCM ambaye alimvamia mgombea wa Chadema wa nafasi ya
ujumbe, Stephen Mgombozi na kumrushia
maneno kwamba alikuwa ana mtafuta sana na kuanza kumshambulia kwa kumpiga na kupiga
teke sanduku la kura.
Baada ya hapo hali ya amani
ilitoweka kwani vurugu zilikuwa kubwa kwa baadhi ya wafuasi na viongozi wa
vyama hivyo hasimu kuchapa makonde hali iliyowalazimu Polisi kuingilia kati.
Akizungumzia vurugu hizo Magwiza,
alisema mawakala wawili wa Chadema wanashikiliwa na Polisi kwa madai ya kuvunja
masanduku manne ya kura na hivyo kusababisha vurugu zaidi kutoka kwa wafuasi na
viongozi wa CCM.
Alisema tafrani hiyo
iliwafanya Polisi kuwatawanya wapiga kura kwa mabomu ya machozi na risasi za
moto hewani.
Aidha, baada ya vurugu hizo
aliwasiliana na Msimamizi wa Uchaguzi, Mussa Natty, ambaye ni Mkurugenzi wa
Manispaa ya Kinondoni kuhusu hali hiyo.
“Hii amri ya kuahirisha
chaguzi ni agizo la Mkurugenzi lakini hata hivyo tulishauriana na vyama vyote
viwili na tumetiliana saini ya makubaliano ya kuahirisha uchaguzi huu hadi utapotangazwa
tena,” alisema Magwiza.
Alisema uchaguzi huo utafanyika
tena kama uchaguzi mdogo ambao utapangiwa siku ya kufanyika na Ofisi ya Tawala
za Miokoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Hata hivyo, Msimamizi huyo,
alisubiri kutoa tangazo hilo hadi alipofika Kamanda Polisi wa Operesheni Tile,
ambaye alipewa taarifa na msimamizi huyo kisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo.
Katika eneo hilo kulikuwa
na kikosi cha polisi huku wakiwa wamejihami na silaha za moto na mabomu ya
machozi ambao walifika hapo wakiwa katika magari mawili.
Katika kituo cha uchaguzi cha
Kigogo Fresh Pugu, hadi majira ya saa
saba mchana, wananchi walikuwa hawajaanza kupiga kura na hakuna sababu zilizotolewa.
No comments:
Post a Comment