Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya sikukuu ya Christmas, wataalam wameonya kuwa kuwapa zawadi nyingi watoto kuna madhara na kwamba wazazi wasiwape kila wanachotaka.
Wamedai kuwa kuwapa zawadi nyingi watakuwa wanatengenezea watoto wao matatizo wakiwa wakubwa.
Watafiti wa chuo kikuu cha Missouri wameonya kuwa kununua zawadi nyingi kwa watoto kunaweza kuwafanya wawe wapenda mali na matatizo mengi ya kitabia siku za usoni.
‘Utafiti wetu umebaini kuwa watoto wanaopokea zawadi nyingi kutoka kwa wazazi wao wana uwezekano wa kuwa na tabia za anasa wakiwa wakubwa na hii inaweza kuwa na matatizo,” alisema Marsha Richins aliyeongoza utafiti huo.
No comments:
Post a Comment