HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » BALOZI SEIF AKABIDHI MABOMBA YA MAJI YENYE THAMANI YA MILIONI 17 KWA AJILI YA KIJIJI CHA KILOMBERO, UNGUJA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Mabomba ya kusambazia maji safi Diwani ya Wadi ya Upenja Bibi Asha Abdulla Mussa kwa ya Kijiji cha kilombero Mkoa wa Kaskazini Unguja. Kati kati yao ni Mke wa Balozi Seif Mama Asha Suleiman Iddi.

Mabomba ya kusambazia maji safi katika Kijiji cha Kilombero yenye gharama ya shilingi Milioni 17,000,000/- yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kitopo Balozi Seif Ali Iddi.

Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akishiriki katika kazi ya uchimbaji mtaro kwa ajili ya ulazaji wa mabomba kwa ajili ya huduma za kusambazia maji safi katika Kijiji cha Kilombero. Picha na Hassan Issa wa – OPMR – ZNZ.

Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi alisema licha ya juhudi zinazochukuliwa na viongozi katika kuchangia nguvu za kukabiliana na matatizo mbali mbali yanayowakabili wananchi katika maeneo yao lakini bado jukumu hilo litaendelea kubakia mikononi mwa wananchi wenyewe.

Alisema Viongozi na hata Serikali Kuu huhamasika na kushawishika zaidi kusaidia hata uwezeshaji na hata vifaa kwenye miradi ya Jamii baada ya kuona nguvu za Wananchi zimeanza au kuiendelezwa katika kujikomboa na umaskini au kujitafutia maendeleo yao.

Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema hayo wakati akikabidhi mabomba 250 ya kusambazia huduma za maji safi na salama kwa ajili ya Wananchi wa Kijiji cha Kilombero hapo katika kituo cha Kilimo Kilombero Wilaya ya Kaskazini “ B “ Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Mabomba hayo yaliyogharimu jumla ya shilingi Milioni 17,000,000/- nusu ya gharama ya fedha hizo imetokana na mfuko wa Jimbo ( CDF ) na nusu iliyobakia imetolewa na Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope.

Balozi Seif pia alishiriki kazi ya uchimbaji mtaro wa ulazaji wa bomba hizo unaoanzia kwenye kisima kilichochimbwa kwa ajili ya mradi huo wa usambazaji maji ambacho kimeshakalimika uliokwenda sambamba na upatikanaji wa huduma za umeme katika kisima hicho.

Aliwapongeza wananchi wa Kijiji cha Kilombero kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya ya kujiondoshea matatizo yanayowakabili ikiwemo kushiriki katika kazi za usambazaji wa huduma za maji safi.

Balozi Seif alisema huduma za upatikanaji wa maji safi ni zao hivyo lazima wahakikishe wanashiriki kwa nguvu zao zote katika kukabiliana na changamoto kama hizo za jamii.

Aliwaeleza wananchi hao wa Kijiji cha Kilombero kwamba jitihada zitaendelea kuchukuliwa na Uongozi wa Jimbo hilo za kusambazwa huduma za maji safi na salama katika mitaa ya kijiji hicho mara baada ya Bomba za maji hayo kufikishwa katika eneo la Skuli ya Kilombero kutoka kwenye kisima hicho.

“ Suala la tataizo la huduma za maji safi ndani ya kijiji cha Kilombero litaendelea kubakia katika historia siku chache zijazo “. Alisema Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi.

Aliendelea kuwaasa wananchi hasa vijana kujiepusha na tabia ya kushawishiwa na baadhi ya Watu wakiwemo wanasiasa katika kujiingiza kwenye uchochezi unaozaa balaa na matatizo.

Balozi Seif alisema ni vyema kwa wananchi hao wakalazimika kuelewa athari ya uchochezi unaofanywa na wanasiasa hao ambao mara nyingi unalenga kuwanufaisha wao binafsi.

Mapema Diwani wa Wadi ya Upenja Bibi Asha Abdulla Mussa akipokea mchango wa mabomba hayo ya usambazaji maji safi katika Kijiji cha Kilombero alimpongeza Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope kwa moyo wake wa kusaidia kuondosha matatizo yanayowakabili wananchi wa Jimbo lake.

Diwani Asha alimuomba Mbunge huyo kuendelea na juhudi hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikileta faraja kwao Viongozi wa wadi na Matawi yaliyomo ndani ya Jimbo hilo pamoja na wananchi wote.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji cha Kilombero Msimamizi wa Kamati ya mradi wa Maji ya Kijiji hicho Bwana Moh’d Haji Faki alimuhakikishia mbunge huyo wa Jimbo la Kitope kwamba Wananchi wa Kijiji hicho wako tayari muda wowote kushiriki katika kazi za maendeleo wakati watapotakiwa kufanya hivyo.

Bwana Moh’d alisema mradi huo wa usambazaji huduma za maji safi katika Kijiji hicho ni miongoni mwa kazi hizo ambazo wataendelea kushirikiana katika kuzitekeleza kwa faida yao na ustawi wa vizazi vyao.

Zaidi ya shilingi Milioni 20,000,000/- zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi zimetumika katika ujenzi wa Kisima cha Maji ya Kilombero kwa lengo la kuwaondoshea usumbufu wa miaka mingi wa huduma za upatikanaji wa maji safi na salama wananchi wa Kijiji hicho.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: