Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Afisa Miradi wa ForumCC Fazal
Issa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo
Mwezeshaji kutoka Youth Can Tanzania, Rahma Mwita, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo
Afisa Miradi
huyo amesema katika mkutano huo wa Peru kulikuwa na makundi mbalimbali kutoka
kila pembe ya dunia yakiwamo kundi la nchi za Afrika ambazo ndizo zimekuwa
muathirika mkubwa wa mabadiliko ya tabianchi. Mkutano huo pia ulizikutanisha
nchi 72 zilizokwenye kundi la nchi zilizoendele na ambazo ni chanzo kikuu cha
uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa na viwanda vinavyozalisha
hewa ukaa na kuongeza joto duniani.
Aidha Afisa huyo amesema kuwa kulikuwa na kundi kutoka nchi za Bara la Asia
na kundi la nchi za visiwa pamoja na makundi mengine ya wanaharakati wa
mazingira ambao walipigana kuzibana nchi zilizoendelea kupunguza uharibifu na
kutoa pesa kwa nchi zilizoathirika na
zinazoendelea kuathirika na mabadiliko ya tabianchi.
Amesema nchi
zinazoendelea ikiwamo Tanzania walikuwa na msimamo mmoja ambao ni kupunguza
gesi joto duniani , na kuzitaka nchi zenye viwanda kutoa fedha zaidi katika
mfuko wa pamoja wa mazingira katika kujenga uwezo kwa nchi maskini na
zinazoathirika kupunguza na kumaliza changamoto za mabadiliko ya tabianchi
“Zinahitajika
dolla bilioni 100 kwa mwaka katika kushughulikia mabadiliko ya tabianchi
duniani na kiasi kilichochangwa ni dolla
bilioni 10 sawa na asilimia 10% tu ya fedha ambazo zinazohitajika, Utaona hapo ni kwa kiasi gani
nchi zilizoendelea zinahitajika
kuchangia mfuko huu” anasema Fazal.
Afisa Habari ForumCC, Tajiel Urioh akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo
Waandishi
wa habari wakifuatilia taarifa ya mrejesho wa yaliyojiri kwenye Mkutano
wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi COP20 uliofanyika Peru mwishoni
wa mwaka jana.
Naye katibu mkuu
wa asasi ya kiraia ya (Youth-CAN) Justine Mponda amesema wao kama vijana
wapambanaji wa mazingira hapa nchini wameshiriki katika mkutano huo wa COP 20
Peru kwa lengo la kujifunza zaidi kutoka
kwa vijana wenzao duniani walioshiriki katika mkutano huo wa mabadiliko ya
tabianchi.
“
tunajihusisha na kutoa elimu ya
mabadiliko ya tabianchi kwa jamii juu ya
athari ya mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na kuwashawishi vijana nchi juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Pia kufikisha madai na vilio vya vijana nchini waathirika wa mabadiliko ya tabia nchi kwa
serikali na taasisi za kimataifa kwa utatuzi zaidi”
Taasisi hiyo ya Youth –CAN ina lengo la kufanya kampeni nchini
kabla ya mkutano wa mabadiliko ya tabianchi wa mwaka huu Paris Ufaransa. Kmpeni yenye lengo la
kuwafikia watu zaidi ya milioni 1 nchini ambao ni makundi ya vijana, wazee,
wanawake na wanahabari na katika kampeni
hiyo watatumia usafiri wa baiskeli katika ile hali ya kuepuka kuchafua
mazingira.
Mkutano wa
mabadiliko ya tabia nchi maarufu kama COP20 ulifanyika jijini Lima nchini Peru
kuanzia Desemba mosi na kumalizika
Desemba 14 mwaka 2014 ambao ulikuwa na malengo ya kujadiliana na kupitisha maadhimio ya
mkataba ambao utaenda kusainiwa mwishoni
mwa mwaka huu jijini Paris Ufaransa
No comments:
Post a Comment