HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » KUPUNGUZA UMASIKINI KUENDELEA KUWA LENGO KUU LA MILENIA- UN

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Ofisa Habari Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na washiriki wa Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ofisa Habari Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na washiriki wa Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wananchi waslioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wananchi walioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali walioshirii atika Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali walioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwakatika maumbo ya kuunda neno '2015' kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu 
OFISA Habari Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema bado lengo la kupunguza kiwango cha umasiki lililokuwa katika malengo ya milenia yaliyomalizika mwakani litaendelea kuwa changamoto kwa nchi mbalimbali kutokana na hali ya utekelezaji wake. Bi. Nkhoma ametoa ufafanuzi huo Uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam katika Uzinduzi wa Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015 zilizozinduliwa leo Dar es Salaam.
 Alisema jitihada zinafanyika na nchi mbalimbali zipo katika viwango tofauti katika kulitimiza lengo hilo. "...Kwanza lazima tukubali kuwa ni lengo ambalo linachangamoto kubwa kiutekelezaji karibia nchi nyingi, hivyo litaendelea kupewa uhimizaji kiutelekezaji hata katika malengo yajayo," alisema Bi. Nkhoma. 
 Hata hivyo akizungumzia suala la kupunguza maambukizi ya Ukimwi alisema bado ni lengo ambalo linachangamoto kubwa licha ya kwamba maambukizi mapya bado yapo lakini nguvu kubwa imewekwa katika kupunguza hayo maambukizi mapya. "...Tupunguze maambukizi mapya na tusiwe tena na watu wanaoendelea kufa kutokana na maambukizi ya Ukimwi...hili bado ni lengo ambalo linaendelea kufanyiwa kazi kwa nguvu kubwa pia linahitaji msukumo na jitihada za mtu mmoja mmoja, lakini pia kama nchi, kama taifa na jumuiya za kimataifa katika kupambana nalo," alisema.
 Alisema lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga na wajawazito bado ni lengo lenye changamoto, hii ni kutokana na suala hili utekelezaji wake unahitaji rasilimali ya kutosha kuhakiisha tuna hospitali, vituo vya afya na klinii za kutosha kuhakikisha tuna sehemu za kutolea huduma kwa akina mama na watoto. Hospitali zetu kuwa na vifaa na wahudumu wa afya waliosomea na kubobea kwenye huduma hizo. "Bado kuna changamoto lakini tutatumia changamoto zilizokuwa katika utekelezaji kwa miaka iliyopita kutatua changamoto za sasa kimaboresho zaidi. Kupunguza umasikini sio suala la sera bali ushiriki wa wananchi mmoja mmoja oale alipo, pia hili ni suala mtambuka kutokana na kutegemeana na sekta nyingine. 
Mfano mkulima hawezi kupunguza umasikini kama hana pembejeo, kama hana miundombinu imara ya kusafirisha mazao yake kutoka shambani hadi sokoni na pia kupata soko la uhakika anapoingiza mazao yake sokoni." Alisema ili kupambana na hili inabidi kujengwa mazingira kuhakikisha kila mmoja anashiriki kupambana na malengo hayo, mfano fursa za ajira na fursa za kujiajiri haiwezekani kila mtu kuajiriwa so inabidi kuandaliwa wengine kujiajiri wenyewe. "...Sio lazima kila mtu aajiriwe kila mtu anakipaji chake katika uzalishaji kinaweza kutumika kwa kuendelezwa na kujikuta anafanya vizuri," alisema. 
 Kampeni ya Chukua Hatua Dhidi ya Umasikini 2015 zimezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam na kushiriisha makundi mbalimbali, wazee, vijana, wanafunzi wa Msingi na Sekondari, watu wenye ulemavu na makundi mengine husika. Imeandaliwa na www.thehabari.com

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: