Ndugu wasomaji wetu
tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili
tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba
+255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mwenyekiti wa Chuo cha Karate nchini Tanzania,Willy Ringo leo ameyataka mashirika na makampuni nchini kuunga mkono mchezo wa Karate ili kufika mbali zaidi ulimweguni.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,Rwezaula ameitaka Serikali pamoja na Makampuni yeyote kuusaidia mchezo huo wa Karate,pia ameitaka Serikali kuacha kudhamini michezo mingine kama mpira wa miguu na mashindano ya urembo.
Kwa upande wake, Bingwa wa Dunia katika mchezo wa Karate, Rutashobya Ringo amewataka Watanzania kuwa na nidhamu pamoja na kumuamini Mungu katika mchezo wowote ili kujihakikishia ushindi.
Mwenyekiti Chuo cha Karate Tanzania Willy Ringo Rwezaula akionesha mmoja cheti alichokipata baada ya kushinda moja ya mashindano nje ya nchi ndugu Rutashobya Ringo leo jijini Dar es Salaam
Rutashobya Ringo akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar baada ya kuonesha vyeti vyake pamoja na kombebaada ya kushinda kombe la Karate nchini Urusi. Pia ameeleza kuwa anakwenda kushiriki olympic nchini Brazil kwenye mshindano ya Karate.
Bwana Dormidontov Vadim ambaye ni mwalimu wa mchezo wa Karate nchini Urusi akizungumza jambo na waandishi wa habari leo jijini Dar
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini
Rutashobya Ringo akionesha umahiri wake katika mchezo wa Karate
Mwalimu wa mchezo wa Karate nchini Urusi, Bwana Dormidontov Vadim akionesha umahiri wake kwenye mchezo huo mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani)
No comments:
Post a Comment