Ndugu wasomaji
wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei
nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi
kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime – SACP akiongea wakati wa kufunga mafuzo kwa waendesha pikipiki (Bodaboda) wa Manispaa ya Dodoma yaliyoendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la –APEC - kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mafunzo yaliyochukua wiki moja kuanzia tarehe 12/01/2015 hadi tarehe 19/01/2015.
Bw. Erasto Kasugu
akisoma risala kwa mgeni rasmi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi David Misime
(hayupo pichani).
Mkurugenzi Mtendaji wa APEC Bw. Respicius Timanywa
akiongea jambio kwenye ufungaji wa mafunzo kwa waendesha
pikipiki (Bodaboda) wa Manispaa ya Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi David Misime
– SACP akikabidhiwa zawadi na waendesha pikipiki(Bodaboda).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi David Misime
– SACP akikabidhi vyeti vya mafunzo kwa washiriki.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakisikiliza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi David Misime– SACP akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi toka Jeshi la Polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi David Misime – SACP akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa shirika la APEC.
Na. Sylvester Onesmo wa
Jeshi la Polisi Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
kwa kushirikiana na wadau wengine litaendeleza msako kwa wale wote waendesha
pikipiki ambao hawana leseni kwani walishapewa muda mrefu ili waweze kupata leseni pamoja na mafunzo ya udereva.
Ameyasema hayo wakati wa kufunga mafuzo kwa waendesha
pikipiki (Bodaboda) wa Manispaa ya Dodoma yaliyoendeshwa na Shirika
lisilo la kiserikali la –APEC kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mafunzo
yaliyochukua wiki moja kuanzia tarehe 12/01/2015 hadi tarehe 19/01/2015.
Kamanda MISIME amesema elimu walioipata waendesha pikipiki
(bodaboda) waitumie vizuri ili kujiepusha na ajali ambazo kwa kiwango kikubwa
zinasababishwa na makosa ya kibinadamu na ukosefu wa mafunzo.
Aidha Kamanda MISIME ameeleza kuwa takwimu za kuanzia mwezi
Januari hadi Desemba 2014 zinaonyesha ajali za pikipiki zilikiwa 62, kati ya
hizo ajali za vifo ni 16 ambazo zilisababisha vifo vya watu 18. Pia ajali za
majeruhi zilikua 28 na jumla ya watu 31 walipata majeraha sehemu mbalimbali.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Ant – Poverty and Development Care
(APEC) Bw. RESPICIUS TIMANYWA amesema kutokaa na ajali za barabarani kuwa
nyingi hapa nchini, imebainika kuwa ajali nyingi za vifo na majeruhi ni za
waendesha pikipiki wasio na mafunzo stahiki na utafiti uliofanywa na APEC kwa
Mkoa wa Dodoma umebaini kuwa waendesha pikipiki wengi kutokuwa na elimu ya
usalama barabarani, leseni za udereva na kutokuwepo na mahusiano mazuri kati
yao na Jeshi la Polisi jambo linalosababisha ongezeko la ajali za barabarani na
vurugu.
Pia amezitaja changamoto mbalimbali zilizopo katika kazi ya
APEC ni muitikio mdogo wa walengwa ambao ni madereva wa vyombo vya moto,
madereva wenye leseni bila vyeti vya kutoshiriki mafunzo katika vyuo
mbalimbali.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi kwa niaba ya Katibu wa
waendesha pikipiki (Bodaboda) Manispaa ya Dodoma Bw. ERASTO KASUGU amesema katika mafuzo haya
waendesha pikipiki wapatao 193 kutoka maeneo mbalimbali katika Manispaa ya
Dodoma wamepatiwa mafunzo ya usalama barabarani na pia walieleza changamoto
zinazowakabili ambazo ni kukabwa na kuibiwa pikipiki, madereva wa magari
makubwa hususani malori kutowathamini waendesha pikipiki wanapokuwa barabarani,
baadhi ya abilia kukataa kuvaa helmet, baadhi ya waendesha pikipiki kuvaa jina
la bodaboda huku wakifanya vitendo vya uhalifu pamoja na baadhi ya waendesha
pikipiki kukataa kushiriki mafunzo ya usalama barabarani kama yaliyotolewa na
APEC.
Aidha wamesema kwa kuwa wamepata mafunzo ya Polisi Jamii na
mbinu za kuwakamata waalifu, wameomba ushirikiano mkubwa pindi wanapotoa
taarifa za matukio yasiyofaa baada ya kuwatilia shaka au kuwabaini waarifu.
No comments:
Post a Comment