HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » RAIS KIKWETE AKABIDHI VITABU 201 KWA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI, AAGANA NA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA NA RWANDA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange alipokuwa akimshukuru kwa kutoa vitabu  kwa Chuo cha Ulinzi na makataba zingine za JWTZ wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vitabu 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha Ulinzi (National Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam jana Ijumaa January 9, 2015.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi baadhi ya vitabu   na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange. Rais Kikwete amekabidhi vitabu hivyo 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha Ulinzi (National Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam jana Ijumaa January 9, 2015. Rais kikwete, ambaye ameshachangia jumla ya vitabu 2752 katika maktaba ya chuo hicho na maktaba zingine za JWTZ  katika vipindi tofati, amesema elimu imo vitabuni, na ili kuelemika yapaswa mtu usome vitabu, na kwamba taasisi ya elimu inakamilika ikiwa na vitabu.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na maafisa waandamizi wa JWTZ wakiangalia vitabu wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vitabu 201 kwa ajili ya Maktaba ya Chuo cha Ulinzi (National Defence College - NDC) iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam jana Ijumaa January 9, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mhe Jacky Zoka, Balozi wa Tanzania nchini Canada na Mhe Ali Siwa, Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, walipofika Ikulu jijini Dar es salaam jana Ijumaa January 9, 2015 kuaga rasmi kabla ya kwenda kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi. 
PICHA NA IKULU.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: