HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » WANANCHI SONGEA WALALAMIKIA TATIZO LA UMEME KWA MIEZI MITATU SASA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Wananchi  wa manispaa ya songea mkoani ruvuma wamelalamikia tatizo la umeme lililoukumba mji wa songea kwa zaidi ya miezi mitatu sasa baada ya kuharibika mitambo ya kuzalisha umeme tangu Oktoba mwaka jana na kusababisha  mgao mkali wa umeme katika mji huo.
Wametoa malalamiko hayo wakati wakizungumza na ITV kuhusiana na tatizo la umeme katika mji wa songea  na  kusema tatizo hilo limesababisha maisha yawe magumu.
 
Meneja wa uzalishaji wa umeme wa nishati ya mafuta na gesi nchini
Mhandisi Gregory  Chegelle amesema mafundi wanajitahidi kufufua mitambo iliyokufa na kwamba  mji wa songea utarejea katika hali yake ya kawaida ya umeme mwezi februari mwaka huu watakapokamilisha matengenezo ya mitambo Hiyo.

CHANZO: ITV TANZANIA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: