Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Sehemu
ya barabara ya Ndundu –Somanga(KM 60) iliyokamilika kwa kiwango cha lami
Wanahabari wakimhoji Dereva wa basi la abiria kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam kuhusiana na kukamilika kwa sehemu ya barabara hiyo.
Habari na picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kukamilika kwa barabara ya Ndundu- Somanga (Km 60) na kuwataka wakazi wa mikoa ya kusini kuitumia vizuri barabara hiyo kuibua fursa za kiuchumi na hivyo kujiletea maendeleo.
Dkt. Magufuli alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kukamilika kwa ukaguzi wa barabara hiyo uliofanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe.
“ Wito wangu kwenu wakazi wa mikoa ya kusini ni kuitunza barabara hii ili idumu kwa muda mrefu na kuibua fursa za kiuchumi zitakazo wawezesha kupata maendeleo na kupunguza umaskini” alisisitiza Waziri Magufuli.
Kufatia kukamilika kwa barabara hiyo, Dkt. Magufuli ameishukuru Wizara ya Ujenzi pamoja na Wakala wa Barabara Nchini, (TANROADS), kwa kazi kubwa ya kusimamia kazi hiyo iliyodumu kwa muda mrefu kutokana na changamoto mbalimbali.
“Nampongeza Katibu Mkuu wa Wizara pamoja na Mtendaji Mkuu wa TANROADS kwa usimamizi makini uliosababisha kukamilika kwa mradi huu muhimu utakaoleta ukombozi kwa wakazi wa mikoa ya kusini” alisema Waziri Dkt.Magufuli
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe ameelezea kuridhishwa kwake na ujenzi wa barabara hiyo na kuwaomba wananchi kuitunza ili idumu kwa muda mrefu.
“Barabara hii imekamilika kwa kuchelewa lakini imezingatia viwango vilivyowekwa kimkataba hivyo nawasihi madereva na wananchi kuitumia kwa uangalifu ili kuepuka ajali na kuibua fursa za maendeleo” alifafanua Eng. Iyombe
Barabara ya Ndundu-Somanga ni sehemu ya barabara kuu ya Dar-Es-salaam -Lindi-Mtwara ambayo imekuwa kwenye matengenezo kwa muda mrefu na Ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 60.
No comments:
Post a Comment