Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa
kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo
lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru
kwa ushirikiano wenu.
Baadhi ya Wajumbe wa Serikali za Mitaa waliopatikana katika Uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kutoka katika Majimbo ya Ilala,Ukonga na Segerea wakila kiapo mbele Wakili wa Serikali kwenye Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa waliopatikana katika Uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kutoka katika Majimbo ya Ilala,Ukonga na Segerea wakila kiapo mbele Wakili wa Serikali (hayupo pichani) kwenye Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.
Sehemu ya Wenyeviti na Wajumbe wao wakiwa nje ya Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo wakisubiria kuitwa majini yao kwa ajili ya kwenda kula viapo.
Sehemu ya Wenyeviti na Wajumbe wao wakijaza fomu za viapo kabla ya kuapishwa.
Na Chalila Kibuda
Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa wa wa Kwalala na Kigogo Fresh B
wa Chama cha Mapinduzi (CCM)waameshindwa kuapa kuwa mwenyekiti wa kutokana na kudaiwa sio wa washindi katika
nafasi hiyo.
Zuio la kushindwa kuapishwa
kwa viongozi hao kulizua mgogoro kati ya chama cha CCM na Chadema na
kulazimika Jeshi la Polisi kuwaondoa viongozi hao.
Wenyeviti hao ni Mariano Maurus CCM na Patriacian Mamakula Chadema ,kila mmoja
anadai ndiye mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Kigogo Fresh B.
Katika Mtaa wa Kwalala wagombea ni Doricasy Lukiko wa
Chadema na Khadija Sidemoga wa CCM wote wanadai kuwa wameshinda uchaguzi wa
serikali ya Mtaa huo katika nafasi ya Mwenyekiti.
Mariano Maurusy alisema yeye
ndiye mshindi wa Mtaa wa Kigogo Fresh alimshinda Patrician Mamakula wa Chadema
,kuwa CCM ilipata kura 233 na Chadema kura 228.
Alisema kuwa wanachama wa Chadema
walifanya vurugu katika uchaguzi huo kwa kuchoma kura bila kujua msaidizi wa
uchaguzi alikuwa na nakala zinazoonyesha ushindi wa mwenyekiti na wajumbe wa
CCM.
Wanachama wa Chadema walidai
kuwa anayejiita mshindi kwa tiketi ya CCM ni muongo wanapoteza ukweli juu ya
uchaguzi huo kwa kuaminisha wameshinda kumbe sivyo.
CHANZO: MICHUZI BLOG
CHANZO: MICHUZI BLOG
No comments:
Post a Comment