Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikata utepe katika ufunguzi wa ZuRii House of Beauty duka jipya na la kisasa la vipodozi lililofunguliwa rasmi leo Jumatatu 12 Jan 2015 kulia ni Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akifungua duka rasmi.
ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akitoa ufafanuzi kwa Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige kuhusu bidhaa zilizopo kwenye duka la ZuRii Fashion & Beauty Boutique
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akizungumza na vyombo vya habari kwenye ufunguzi wa duka hilo la vipodozi
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliofika kufanya manunuzi ndani ya duka hilo
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George( kulia) akiwa na mwana harakati mwenzake Shamim Mwasha mmiliki wa blog ya 8020.
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akitoa ufafanuzi kuhusu ufunguzi na ujio wa duka hilo hapa nchini Tanzania likiwa na muonekano tofauti
Mmoja wa wateja waliofika katika duka hilo akitizama bidhaa
Muonekano wa duka la Zurii kwa ndani
Baadhi ya Bloggers wenzake waliofika kumpa support mwenzao kwenye ufunguzi wa duka la vipodozi
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Viti Maalum
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Vijana , Mkoa wa Arusha Catherine Magige leo amezindua rasmi duka
jipya la vipodozi na vitu mbalimbali linalofahamika kwa jina la ZuRii
lililopo katika jengo la Dar Free Market lililopo katika barabara ya Alli
Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.
Akizindua duka hilo
ambalo linamilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina
George, Magige alisema kwamba amevutiwa na namna Jestina alivyoweza kurudi na
kuwekeza nyumbani hali ambayo imeweza
kuzalisha ajira kwa watanzania na kuwa mfano wa kuigwa.
“Kabla ya yote nachukua
fursa hii kumpongeza Jestina kwani ameonesha mfano
wa umuhimu wa kujiajiri hasa kwa wanawake pia huu ni mfano wa
kuigwa kwa wanadiaspora , wengine warudi
na kuja kuwekeza nyumbani kwani fursa nyingi zipo hivyo waje wazitumie” alisema
Magige.
Aidha alitoa rai kwa
wanawake wengine hapa nchini ambao wanauwezo wa kuwa na mitaji ya kuanzisha
biashara wajiajiri na kutoa ajira kwa wengine
pia natoa wito kwa watanzania wengine waje katika duka la ZuRii kuja
kutoa sapoti kwa Jestina, alisema Magige.
Wakati huohuo mmiliki
wa duka hilo la ZuRii Jestina alisema
kwamba yeye ameona fursa za kuwekeza nyumbani hivyo ameamua kuzitumia ipasavyo.
“Natoa wito kwa kwa wanadiaspora
wenzangu ni kwamba wasiwe na tabia za kuja likizo nyumbani nakuinjoi tu fedha zao tu bali wajitahidi kuja kuwekeza
kwani fursa zipo, kuanzisha duka hili ni ndoto yangu ya siku nyingi hivyo haya
ni matokeo ya njozi yangu namshukuru Mungu
kwa kutimiza ndoto hii”.
No comments:
Post a Comment