Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mbunge wa Bariadi Magharibi, Adrew Chenge akihojiwa na Baraza la Maadili la Viongozi wa Umma leo.
Prof. Anna Tibaijuka akiwa mbele ya wajumbe wa Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma akisomewa tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Prof. Anna tibaijuka akiwa mbele ya jopo la wajumbe wa Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma wakati akihojiwa leo kuhusiana na mgano wa fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.
Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka (kushoto) akiwasili katika ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya kuhojiwa na Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na mgao wa fedha zilizokwapuliwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow. (Picha na Francis Dande)
Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji mstaafu Hamis Msumi akitafakari jambo.
Wakili wa Prof. Anna tibaijuka Dk. Rugemeleza Nshala akimuuliza maswali shaidi wa upande wa serikali.
Wakili Dk. Rugemeleza Nshala na Prof. Anna Tibaijuka wakipitia nyaraka wakati Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma lilipoketi na kumuhoji aliyekuwa Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusiana na mgao wa fedha zilizokwapuliwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Adrew Chenge wakati akitoka kuhojiwa na Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kuhusiana na mgao wa fedha zilizokwapuliwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
Mbunge wa bariadi Magharibi Adrew Chenge akitoka katika ukumbi wa Karimjee mara baada ya kukutana na wajumbe wa Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma.
No comments:
Post a Comment