Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania
Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama (Chid Benzi) amehukumiwa kifungo cha
miaka mwili jela au kulipa faini ya shingili laki tisa bada ya kupatikana na
hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye
thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko
na kigae.
Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa hayo.
Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita,
alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye
tamasha la muziki.
Hata hivyo, Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo
imemwachia huru mwanamuziki
huyo baada ya kulipa faini ya 900,000/
No comments:
Post a Comment