Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Gari dogo aina ya Toyota RAV4 limepinduka leo katika kijiji cha Mbela wilayani Misungwi, mkoani Mwanza na kujeruhi watu kadhaa waliokuwa ndani yake baada ya kumshinda dereva wake wakati lilikata kona na hivyo kuanguka katika bonde la daraja.
Wasamaria wema wakitoa msaada.
Kwa mujibu wa mashuhuda, gari hilo lenye usajili wa T 358 CBA mali ya Machalo Joseph, lilikuwa likiendeshwa na Festo Kakula wa Misungwi, na baada ya ajali majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Mitindo wilayani Misungwi.
No comments:
Post a Comment