MOTO WAZUKA HOSTELI ZA MABIBO JIJINI DAR LEO ASUBUHI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Kwa taarifa ambazo zimetufikia muda huu zinadai kuwa Bweni la Mabibo Hosteli jijini Dar es Salaam linaungua moto muda huu, bado sababu na chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.
Katika tukio hilo wanafunzi wawili wamekimbizwa hospitali baada ya kuumia katika purukushani za kujiokoa ambapo mmoja alijirusha kutoka ghorofa ya pili ulipoanzia moto huo na mwingine aliumia kwenye mkanyagano wakati wa kujiokoa.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI



Jengo  la ‘Block B’  la Hostel za Mabibo,  za wanafunzi wa kike wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), jijini Dar es Salaam limeungua kwa moto na kuteketeza vifaa na mali kadhaa  za wanafunzi waliokuwa wakiishi kwenye jengo hilo.
Tukio hilo lililotokea leo majira ya 2:35 asubuhi linadaiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme  katika jingo hilo. Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala aliyekuwa eneo la tukio akiahidi kubeba dhamana ya kushughulikia hasara ya mali, nyaraka na fedha kwa wanafunzi walioathiriwa na tukio hilo.
“Kwanza kuhusu vyeti vilivyoungua ,tutashughulikia vipatikane vyote. Pili tutashughulikia hata bajeti za kujikimu kwa wale walioathirika, lakini pia kuanzia leo wanafunzi wote ambao walikuwa kwenye jengo hilo watahamishiwa jengo lingine wakati huo uchunguzi ukifanyika kufahamu chanzo cha moto,” alisema Profesa Mukandala.
Kwa upande wake, Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alitoa tahadhari ya usalama kwa mali za wanafunzi walioathiriwa na tukio hilo huku akisisiza utulivu wakati uchunguzi wa chanzo hicho ukifanyika. Taarifa kutoka miongoni mwa wanafunzi hao zimebainisha kuwa, wakati wa tukio hilo wanafunzi wawili wa kike waliruka kutoka gorofa ya pili mpaka chini na kujeruhiwa vibaya.
Askari wa Zima Moto walifika eneo la tukio hilo saa 3:45 asubuhi na kukuta moto ukiwa umeshapungua hatua iliyosababisha wanafunzi hao kuwashambulia huku wakiwazomea  na kuwataka waondoke. Viongozi wawili wa zima Moto, Omary Katonga kutoka Ilala na Mboke Msami wamesema changamoto kubwa iliyojitokeza ni kutopata taarifa mapema.
“Moto umetokea saa 2:35 asubuhi kwa nini watujulishe tena kupitia Tanesco saa moja baadaye, tumefika hapa kwa kutumia dakika 23, wanakosea kutulaumu ila kinachotakiwa ni taarifa mapema,” amesema Katonga.

No comments

Powered by Blogger.