Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Kama utakumbuka, kuna wakati niliandika makala inasema malengo hubadilika ila utu wako haubadiliki, haiko peke yako. Je! unaogopa kubadilisha malengo ya kazi unayofanya? Hapa nitakueleza baadhi ya vitu ambavyo naendelea kujifunza, kubadilisha mawazo ni tofauti kabisa na kukata tamaa.
Nimekuwa nikifikiria kuhusu mipango na malengo na namna ya kuyaweka sawa na kwa namna gani unaweza kuyafikia.
Wengi wetu tunajua, ukiwa umewahi kushindwa au kufeli ni kutokana tu labda uliwaza tofauti ni kile ambacho ulitakiwa kutilia mkazo hivyo kuishia sehemu ambayo hukuitarajia kabisa.
Lakini bado unaweza kubadirisha maamuzi na namna unavyofikiri kuelekea sehemu nyingine lakini si kukata tamaa.
Kubadilisha mawazo yako ni haki yako kabisa wala hupaswi kuogopa, hakuna anayeweza kuondoa hilo kwako. Hapa kuna maswali machache ambayo unatakiwa kuyajibu kabla ya kubadilisha malengo yako katika kufikiri kwako:
ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
1. Je ni kitu gani kimebadilika?
Maisha yamekuwa yakibadilika badilika, mambo yanabadilika, vitu vinabadilika, Dunia tunayoijua haibaki kama ilivyo. Vile vile vitu unavyovitaka wakati mwingine unahitaji kubadilika.
Hebu fikiri kwa namna hii. Kama unawaza kuacha kazi na urudi shule, hivyo kama umeoa mkeo hatokuelewa kirahisi utatakiwa kuangalia upya maamuzi hayo. Haimaanishi lengo la wewe kurudi shule limekufa bali inakubidi utizame kwa jicho la tofauti lakini ukilenga kufikia malengo yale yale ya kuendelea kusoma.
Hivyo unatakiwa kujua ya kuwa mambo yamebadilika na si kama zamani, na hii hutokea mara nyingi sana. Hofu na mashaka vinakurudisha nyuma, bali unatakiwa kutizama njia mbadala ya kurudi shule bila kuathiri vitu vingine.
2. Moyoni mwako unawaza nini?
Katika mchakato wa kubadilisha maamuzi yako au namna unavyofikiri haitokei kwa haraka. Kama mwanadamu wa kawaida kuna busara iliyopo ndani yako ambayo unatakiwa kuisikiliza. Wakati mwingine unatakiwa kuruhusu ubongo wako na hisia zako zifanye kazi kwa kusaidiana, ukae chini ujiulize na kutafakari kwa makini, je moyoni mwako kuna nini? na uheshimu unavyosikia kutoka ndani yako.
3. Umejifunza nini?
Mpango wa kwanza kitu kama ni mradi, malengo au kazi ni kitu cha kujifunza vizuri na kwa upekee ake kabisa. Je unajua nini kuhusu wewe na maisha yako? na je ulijua nini kuhusu maisha hapo kabla na sasa yakoje? Je ungepata nafasi ya kufanya maamuzi kwa ape ungefanya nini? Je mawazo hayo yanasaidia vipi kukusaidai kubadilisha unavyofikiri?
Kama nilivyosema mwanzoni kuwa hiki ninachokizungumzia si kukata tamaa ya maisha bali kubadilisha mtizamo wa kifikra aliye ndani yako kwa kuleta matokeo bora zaidi. Hii inaonyesha ishara ya kuwa unakua kwa kiwango gani katika fikra zako, hivyo ni hatua ambayo haitatokea ghafla bali ni pale akili yako inapoanza kulishwa vitu sahihi ambavyo vitachangia mabadiliko yako katika maamuzi.
Kitu ambacho unatakiwa kujua ni kwamba vile ulivyo ni matokeo ya namna ulivyoamua kufikiri na kufanya maamuzi, usitafute mchawi au kumlaumu mtu.
No comments:
Post a Comment