HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » BULEMBO AGEUKWA NA WAJUMBE WAKE SAKATA LA KWENDA KWA LOWASSA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mjumbe wa Baraza la Wazazi, Taifa na Mbunge wa Korogwe, Steven Ngonyani 'Prof .Maji Marefu' akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma hii leo juu ya tuhuma za yeye kutajwa na mmoja wa wajumbe wa baraza hilo kuwa aliratibu na kulazimisha baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kwenda kumuona Mbunge wa Munduli na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa. 
Naye Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani, alisema yeye alielezwa kuhusiana na safari hiyo na rafiki yake Vioroka Kajoko. “Nimekuwa katika jumuiya hii kwa miaka 15. Siko tayari kuchaguliwa kiongozi, marafiki wala maadui. Mimi siko tayari  uomba radhi kwasababu sina kosa nililotenda,”alisema Ngonyani. 
Alisema hajawahi kumshawishi mtu wala kumlazimisha mtu kumpenda mtu anayempenda yeye.
 Jackline Ngonyani aliyejitambulisha kwa Lowassa kama 'Maji mafupi' na kutoa salam za shukrai kwa wana Ruvuma kwa jinsi Lowassa alivyo shiriki katika mazishi ya Capt.John Komba lakini jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa alilazimishwa kushiriki katika msafara huo. Lakini wenzake wanasema yeye alikuwa mmoja wa waratibu.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFHA YAPA CHINI
Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi mkoa wa Njombe, Evarist Lupenza,  akizungumza na waandishi wa habari juu ya safari yao kwenda kwa Lowassa. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wzazi mkoa wa Mwanza, Malila Lugoye.



 Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma, Dk. Damas Mukassa, akiwaonesha waandishi wa habari picha ambayo mjumbe mwenzao alisema wamelazimishwa kwenda kwa Lowassa jinsi alivyokula pozi na Lowassa.
*********************
VIONGOZI waliotajwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa, Abdallah Bulembo, kuratibu safari ya baadhji ya wajumbe wa jumuia hiyo na baraza la Wazazi Taifa kwenda kumsalimia Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa leo wamekanusha vikali kuhusika na uratibu wa baraza hilo.
Jana Bulembo aliwashukia wajumbe waliokwenda nyumbani kwa Waziri Mkuu wa Zamani, Edward lowassa,na kumchakingaia fedha na kumshawishi  agombee Urais na kuwataka waombe radhi kutumia jina la baraza hilo na kasha kusubiri  kamati ya maadili.

Wakizungumza hii leo baadhi ya wajumbe hao wamewataja waratibu walioongoza msafara wao kuwa ni pamoja na Katibu wa CCM Wilaya ya Hanang, Vioroka Kajoro na Mjumbe wa baraza hilo kutoka mkoani Ruvuma, Jackline Ngonyani na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma, Dk. Damas Mukassa.

Mjumbe wa jumuiya hiyo kutoka Mkoa wa Njombe, Evarist Lupenza, alisema aliyekuwa akiandika majina ya wajumbe waliokwenda katika ziara hiyo ni Jackline Ngonyani. 

“Niliwasikia wakisema kwa Mzee ni saa tatu, nikawauliza mnataka kwenda wapi, wakaniambia kuwa wanataka kwenda kumsalimia Lowassa, name nikaandikisha jina kwa ajili ya kwenda huko,”alisema Lupenza.

Nae Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Mwanza, Malila Lugoye alibainisha kuwa hakuna mtu aliyeshinikizwa katika safari hiyo na ilikuwa ni huru kuamua kwenda au kubaki.

 “Hakuna mtu aliyeshinikizwa kwenda kwa Lowassa kila mtu alikwenda kwa mapenzi yake. Na hakuna mtu aliyetumia jina la Jumuiya wakati tulipokwenda bali watu walijitambulisha mmoja mmoja,”alisema na kuungwa mkono na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mkoa wa Mwanza, Malila Lugoye.

Naye Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani, alisema yeye alielezwa kuhusiana na safari hiyo na rafiki yake Vioroka Kajoko.

“Nimekuwa katika jumuiya hii kwa miaka 15. Siko tayari kuchaguliwa kiongozi, marafiki wala maadui. Mimi siko tayari  uomba radhi kwasababu sina kosa nililotenda,”alisema Ngonyani.
Alisema hajawahi kumshawishi mtu wala kumlazimisha mtu kumpenda mtu anayempenda yeye. 

 Dk Mukassa alisema yeye aliratibu ziara hiyo kama mwenyeji wa mkoa wa  Dodoma ambaye anakufahamu nyumbani kwa Lowassa.

 Alisema fedha walizotoa kwa ajili ya kumchangia kuchukua fomu za Sh 600,000 zimetokana na mchango wao wenyewe kama wanachama wa kikundi cha kusaidia cha wajumbe wa jumuiya hiyo.

“Fedha zile hazikutoka kwenye jumuiya ya chama wala hakuna aliyekwenda pale kuwakilisha jumuiya na niliwaeleza pale mliponiuliza na kila mtu alijitambulisha kama yeye,”alisema.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: