Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limekamata gari la kampuni ya Wengert Windrose safari inayojihusisha na uwindaji wa kitalii katika maeneo mbalimbali nchini likiwa linasafirisha madawa ya kulevya aina Bangi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas amesema madawa hayo kiasi cha magunia 11 yamekamatwa katika wilaya ya Longido majira ya saa tano usiku yakisafirishwa kwenda nchi jirani kwenye gari namba T695 ARR mali ya kampuni ya Wengert Safaris ikiwa inaendeshwa na dereva wa kampuni hiyo aliyetajwa kwa jina la Frank Faustine.
Kamanda Sababs amesema polisi walilitilia shaka gari hilo ambalo kwa kawaida linajulikana kuwa linabeba wageni na baada ya kufanya upekuzi ndipo wakagundua kuwa kilichobebwa kwenye gari hilo sio wageni bali ni madawa hayo ya kulevya aina ya Bangi.
ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Akizungumzia tukio hilo meneja maendeleo ya jamii wa kampuni hiyo ya Wengert safaris Bi Aurelia Mtuy amesema madawa yaliyoakamtwa ni mali ya dereva na wala sio mali ya kampuni na amelishukuru jeshi la polisi kwa hatua hiyo ambayo pia imeisaidia kampuni kubaini maovu yanayofanywa na baadhi ya madereva wao.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi pamoja na kulipongeza jeshi la polisi kwa hatua hiyo wameitaka serikali na idara zinazohusika kupanua wigo wa kuweza kubaini mbinu mpya za kihalifu hasa wa usafirishaji wa madawa kwani wana mtandao mkubwa ukiwemo ya kutumia magari ya makampuni, watu maarufu, na taasisi zikiwemo za serikali.
CHANZO :ITV
No comments:
Post a Comment