Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Jeshi la Polisi nchini Tanzania
limewakamata wapigaramli chonganishi 225 katika mikoa ya mbalimbali
ya Tanzania ikiwa ni pamoja na mikoa ya Tabora, Geita, Mwanza,
Simiyu, Shinyanga ambapo kati yao 97 tayari wamefikishwa mahakamani
kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukutwa na vifaa vya uganga ambavyo
vingine ni nyara za serikali kama vile ngozi ya Kenge, meno ya Ngiri,
mikia ya Tumbili, miguu ya Ndege.
Akiongea leo jijini Dar es Salaam,
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Advera John Bulimba amesema watu
hao wamekamatwa kufuatia msako unaoendelea katika mikoa hiyo pamoja
na mikoa ya Kagera, Katavi na Rukwa, ambako pia watu hao wamekamatwa
na mikia ya nyumbu, ngozi ya Simba, ngozi ya Fisi, ngozi ya Digidigi
na wengine kufanya uganga bila kibali.
Advera amesema Jeshi la polisi
litaendelea na juhudi za kukomesha matukio ya kihalifu yaliyoibuka
hivi karibuni ya kuwaua na kuwajeruhi watu wenye ulemavu wa ngozi
(Albino) kwa visingizio vya imani potofu za ushirikina, katika mikoa
yote ili kuhakikisha mtandao mzima unaojihusisha na matukio hayo
unakamatwa wakiwemo waganga wa jadi wanaopigaramli chonganishi.
No comments:
Post a Comment