HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » SUGU AFUNGUKA ASEMA WASANII HAWAKUNISAIDIA KUPATA UBUNGE BALI WALIJIPENDEKEZA CCM

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, amesema hajaweza kufanya kitu chochote kuwasaidia wasanii kwakuwa wakati anagombea ubunge hakuna aliyekuwa nyuma yake. Sugu amelazimika kusema hayo baada ya shabiki kutaka kujua ni kitu gani alichowafanyia wasanii tangu awe mbunge.
“Hao wanaozingua wakamuulize Kikwete studio aliyoitangazia dunia kawapa wasanii iko wapi na kamkabidhi nani,” amehoji Sugu kwenye Instagram. “Rais kashindwa kuwasaidia wanataka kumlaumu mbunge wa Mbeya mjini, wakati hata hao wasanii wenyewe kimsingi hawakutusapoti kwa namna yoyote wakati tunagombea huo ubunge, wote walikuwa wanajipendekeza kwenye kampeni za CCM.”

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: