Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Zitto anatarajiwa kuaga Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutokea misuguano kati yake na Chama chake cha Chadema hali iliyopelekea kubwaga manyanga leo.
Hii inakuja baada ya jana alitangaza kujiuzulu ubunge kwa kusambaza waraka kwa vyombo vya habari.
Baadaye Zitto alikwenda bungeni katika kikao cha jioni kwa ajili ya kuwaaga wabunge wenzake na kuwaeleza sababu za uamuazi wake.
Hata hivyo, kabla ya kuwasili bungeni akisubiri kupewa fursa ya kuwaaga wabunge, aliwaeleza waandishi wa habari kwamba Spika wa Bunge, Anne Makinda amemzuia kuchukua uamuzi huo na kwamba yeye (Zitto) alikuwa akiendelea kumshawishi Spika.




No comments:
Post a Comment