HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA KUANZA TENA SAFARI ZAKE MACHI 24, 2015

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unafuraha kuwataarifu  abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa huduma ya treni ya abiria itaanza upya hapo siku ya Jumanne Machi 24, 2015 kuanzia Stesheni ya Dar es Salaam saa 11 jioni. 

Wananchi wanaotaka kusafiri wafike stesheni zilizo karibu yao kwa ajili ya kukata tiketi ya safari hiyo. 

Huduma ya usafiri wa reli ilisitishwa wiki mbili zilizopita Machi 6, 2015 baada ya eneo la tuta la  reli kati ya Stesheni za Kilosa na Kidete kukuharibiwa vibaya na mafuriko kulikosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha sehemu hizo. 

Kazi ya ukarabati wa eneo hilo iliyokuwa ikifanywa usiku na mchana na Wahandisi na Mafundi wa TRL  ilikamilika siku ya Jumanne usiku Machi 17, 2015.

Halikadhalika muda wa kuondoka treni kwa siku za Jumanne na Ijumaa kutoka Stesheni ya Dar kwenda Kigoma na Mwanza utakuwa saa 11 jioni na zile za kutoka Kigoma na Mwanza kuja Dar  katika siku za Alhamis na Jumapili ni saa 11 jioni  kutokea Kigoma na saa 12 magharibi kutokea Mwanza.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya 
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Mhandisi Kipallo A. Kisamfu
Dar es Salaam
Machi 20, 2015

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: