Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa Tiketi ya Chadema, Kabwe Zitto akisoma barua aliyomwandikia Spika wa Bunge, Anne Makinda kumtaarifu kuwa anang'atuka nafasi ya Ubunge. Pia aliwaaga Wabunge wenzake na kuahidi kurudi tena Mungu akijalia baada ya Uchaguzi wa mwaka huu.
.jpg)
Mhe. Kabwe ametangaza kung'atuka nafasi hiyo baada ya Mwenyekiti wa Bunge Mhe Mussa Hassan Zungu Kumruhusu kutoa kauli binafsi mara baada ya wabunge kumaliza kupitia vifungu vya sheria ya Maafa ambayo hata hivyo haikupitishwa kwa kutotimia idadi ya wabunge ambao nusu yao hawakuwepo ukumbini.

Wabunge mbalimbali wakiwepo wa Chadema, Cuf, NCCR na CCM walionekana dhahiri kububujikwa na machozi kufuatia kujivua kwake Ubunge.
Juu Mheshimiwa Zitto Kabwe na wabunge wengine wakitoka Bungeni mjini Dodoma .
Mhe Zungu alimtakia kila la heri Mbunge huyo machachari ambaye amesema ameamua kuachia ngazi baada ya chama chake kumfukuza. Hata hivyo alimalizia kwa kusema kwamba Mungu akipenda atakuwa nao tena mwezi Novemba mwaka huu. Hakufafanua. Video ya tamko lake hilo hii hapa...
Mhe.Zitto Kabwe akiongea na waandishi wa Habari mara baada ya Kuwaaga Wabunge Baada ya kuwasomea barua aliyomwandikia Mhe.Spika ya Kung'atuka Ubunge baada ya kuvuliwa Uanachama na chama chake cha CHADEMA
.jpg)
Mhe Zungu alimtakia kila la heri Mbunge huyo machachari ambaye amesema ameamua kuachia ngazi baada ya chama chake kumfukuza. Hata hivyo alimalizia kwa kusema kwamba Mungu akipenda atakuwa nao tena mwezi Novemba mwaka huu. Hakufafanua. Video ya tamko lake hilo hii hapa...
.jpg)



.jpg)
No comments:
Post a Comment