Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Hii ndiyo hukumu ya kwanza
kutolewa kwa Morsi tangu aondolewe madarakani, na moja ya hukumu
zinazomuandama. Morsi aliondolewa madarakani na
jeshi mwaka 2013 kufuatia maandamano makubwa mitaani ya kupinga uongozi wake.
Wakati umati ulipokusanyika nje ya
ikulu bwana Morsi aliwaamrisha polisi kuwatawanya lakini wakakataa kufanya
hivyo.Yeye pamoja na viongozi wengine wa Muslim Brotherhood walilaumiwa kwa
kuwachochea wafuasi wao kumuua mwandishi wa habari na waandamanaji wa upinzani
wakati wa makabiliano nje ya ikulu ya rais mwishoni mwa mwaka 2012.
Baadaye Muslim Brotherhood
waliwaleta wafuasi wao ambapo watu 11 waliuawa kwenye makabiliano, wengi kutoka
kwa Muslim Brotherhood.
Kabla ya kutolewa hukumu ya leo,
Muslim Brotherhood walimlaumu rais wa sasa Abdul Fatta al-Sisi kwa kutumia
mahakama kama silaha.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment